Video: Wachina wana mpango gani na nchi yetu? Kuna hii store Mikocheni wanauza kila kitu 3,000. What's going on?

Kwahio wangeuza laki moja ingakuwa sawa ?

Tatizo kubwa unaangalia kinachofanyika kwa ujumla jumla na mwisho wa siku kitu unachokiweka kwamba ni kosa sio kosa...; kwahio elezea makosa (kama ni uhamiaji au kutokulipa kodi) na sio kutoa huduma kwa wananchi ambao serikali na taasisi zao zimeshindwa hivyo angalau kuweza kupata huduma na kubakia na chenji...

Hivi unajua kuna maduka hata huko nje yanatiwa Poundland ? Yaani kila kitu pound moja moja..., au kuna all you can eat buffet ya pound tano au less...; Ukitaka kujua business models zao wanapataje faida takwambia...,; Au unaonaje tungewashukia na WhatsApp kutoka huduma ya calls na mengineyo bure hivyo kuwanyima faranga kina TTCL...

By the way Serikali wakachukue Semina kwa hao Wachina...

 
Ni hivi: Wachina watakuja kufanya nchi isitawalike. Unajua ni wengi hawaoni hili lakini madhara yatakuja kuwapata raia wote, wenye fedha, viongozi na mafukara. Hili jeshi la vijana wasio na kazi ambalo CCM inalijenga litakuja kuisambaratisha nchi.
Hawawezi kukuelewa abadani. Wao adui yao pekee ni CHADEMA, hao wengine hata uhubiri vipi utakuwa unatwanga maji kwenye kinu hadi pale itapokuwa too late.
 
Hiyo ni sawa na YUAN 10 .. China kuna biashara nyingi sana za Yuan 10.. Hapo wanapiga pesa balaa.. Maana vitu vingi hapo havizido Yuan 5
 
Hivyo unavuoshangaa Ndio wasukuma wanavyoshangaaga wakiwa sehem nyingine tofauti na kwao maana uziwa samaki mdogo bukujero nahuyosamaki kwao kule anapewa kamanyongeza
 
Kwani kibanio cha nywele au sahani ya udongo unanunua Tsh ngapi kwenye maduka ya wabongo?

Angalia vizuri hiyo video mkuu. Sio mabanio ya nywele tu, kuna vitu vingi sana.

Kuna vile vikombe aina ya Stanley Cups unakuta vinauzwa 3000.

But that was not my point, my point was, kama biashara ingekuwa rahisi hivyo kwanini wabongo wengi wasingeanzisha nao biashara kama hizo mikocheni.

Unauzaje kitu elfu 3 Mikocheni?
 
Lack of exposure. Maduka hayo yapo kila mahali; na bidhaa zinazowekwa humo zinaendana na bei husika. Unaweza kuta pia bidhaa ghali kidogo lakini zitakuwa zimekaribia kumaliza muda wake na au zipo kwenye promosheni maalum. Usishangae pia kukuta bidhaa chache sana zinauzwa bei ghali kidogo na iliyopangwa. Ni jambo la kawaida sana!



 
Hao ndio wafanyabiashara wanaojua biashara.. wanaona bora wapate faida ndogo lakini wauze sana
 
Serikali inawakumbatia sana hawa kenge, miaka 5 mbeleni tutaanza kujuta na kulaumiana, hakuna uwekezaji wa kipuuzi kama wanaofanya hawa chinese people, hawa watu wanachokifanya ni kureplace bidhaa/biashara za wazawa na kumiliki wao ili miaka ya baadae uchumi wa nchi ushikiriwe na wao, mataifa ya magharibi wanajuta kupoteza muda kuja kuugundua uhuni wa mchina baadae sana.

Na tusivyo na dira ya uongozi thabiti basi huu ndio muda muhimu sana kwao wanautumia kupitisha agenda zao chapuchapu ili tukija kushituka tushachelewa.

Nawaonewa sana huruma vizazi vijavyo maana watatawaliwa na mkoloni mpya ambaye hakuweki utumwani kinguvu bali anakukoloni kiakili kuanzia mali zako mpaka aina ya life style yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…