Video: Wamasai wakiondoka Loliondo

Kama Mkoloni aliwaondoa Serengeti na kuwaleta Loliondo kwa nini unai question Serikali kuwaondoa Ngorongoro na kwenda Serengeti? Au una mawazo ya KITUMWA (Slavery mentality)
Tatizo kuu ni Wamasai kuondolewa katika eneo kwa lengo la kumpa mwarabu wa kampuni ya OBC aliyehonga watawala wetu toka enzi za mzee Ruksa ili apatiwe eneo hilo

Wamasai walipoondolewa Serengeti waliridhia na serengeti haikupewa mtu binafsi. Ila huko Loliondo watawala wanataka kumpa eneo hilo mwana wa mfame wa UAE afanye uwindaji.
 
SSH ni kiongozi makini sana. Huwa anaichukua ile mifupa inayowashinda viongozi wanaomtangulia halafu anaitafuna kwa umahiri wa hali ya juu.

Ni sawa na lile suala la kuhamisha wamachinga mitaani, likaonekana ni gumu sana lakini namna lilivyoshughulikiwa mpaka sasa hivi kumetulia kabisa.

Huu ndio uongozi unaotakiwa, akili na nguvu vinakuwa na uwiano ulio sawa.
 
 

..tatizo la serikali zetu ni KUKURUPUKA.

..hakuna mipango na mikakati ya muda mrefu. miaka mitano baadae usije ukashangaa kuna zoezi jipya la kuhamisha Wamaasai Loliondo.

..Tanapa na NCA ni mashirika yenye ukwasi mkubwa. Kwa maoni yangu walitakiwa wawe na mipango ya muda mrefu na shirikishi ya kudhibiti idadi ya watu na mifugo ktk maeneo yote ya mbuga za wanyama.

..Binafsi sijasikia kama kuna program ya Tanapa / NCA kuwafundisha na kuwawezesha Wamaasai kuwa wafugaji wa kisasa, na kuachana na asili ya kuchunga na kutembeza mifugo kwa malisho.
 
Allegations za kumpa OBC hazina ulweli ni maneno ya kuwatia ndimu wananchi
 
Je ni kweli kuwa hizo kilomita za mraba 1500 ndizo anazopewa huyo mwarabu? mbona hilo hulisemei? Je hulisemei kwa bahati mbaya au
Mwarabu hajapewa hizo 1,500 km bali ana kitalu ambacho ana kodisha na kulipa ushuru toka mwaka 1992.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…