Video: Wamasai wakiondoka Loliondo

Video: Wamasai wakiondoka Loliondo

Kama Mkoloni aliwaondoa Serengeti na kuwaleta Loliondo kwa nini unai question Serikali kuwaondoa Ngorongoro na kwenda Serengeti? Au una mawazo ya KITUMWA (Slavery mentality)
Tatizo kuu ni Wamasai kuondolewa katika eneo kwa lengo la kumpa mwarabu wa kampuni ya OBC aliyehonga watawala wetu toka enzi za mzee Ruksa ili apatiwe eneo hilo

Wamasai walipoondolewa Serengeti waliridhia na serengeti haikupewa mtu binafsi. Ila huko Loliondo watawala wanataka kumpa eneo hilo mwana wa mfame wa UAE afanye uwindaji.
 
Wamasai lazima wahame Ngorongoro. Tufike mahali tutofautishe binadamu na wanyama. Ukweli ni kwamba Ole Sendeka ndiye KUWADI wa wafanyabiashara wa Kenya wanaofugia ng'ombe zao ndani ya Ngorongoro. Maelfu ya ng'ombe waliopo pale siyo ya Wamasai wa Tanzania bali Wamasai wa Tanzania ni vijakazi tu wanaolipwa ujira.

Hiyo Sheria inawanufaisha wakenya na siyo watanzania
SSH ni kiongozi makini sana. Huwa anaichukua ile mifupa inayowashinda viongozi wanaomtangulia halafu anaitafuna kwa umahiri wa hali ya juu.

Ni sawa na lile suala la kuhamisha wamachinga mitaani, likaonekana ni gumu sana lakini namna lilivyoshughulikiwa mpaka sasa hivi kumetulia kabisa.

Huu ndio uongozi unaotakiwa, akili na nguvu vinakuwa na uwiano ulio sawa.
 
Kwa wasioelewa mgogoro huko Ngorongoro na Loliondo.
Ni hivi , Huko Loliondo ndio kuna mwarabu(OBC) anayetaka ardhi ya wananchi, nguvu na ubabe unatumika kuwaondoa watake wasitake.

Eneo la Kilometa za mraba 1500 huko Loliondo ni eneo ambalo yule mwarabu wa OBC analitaka , na ndio figisufigisu zote hizi za kufukuza wananchi ili kumpa huyu mwarabu eneo afanye anavyotaka. Huyu mwarabu ndio Kigwangwallah alipokuwa waziri alisema alitaka kumhonga dola laki moja akakataa

Na kuhusu Ngorongoro, huko ndio wamasai wamejengewa nyumba chache Handeni ili kuwahadaa watanzania kuwa serikali inawajali wamasai kumbe bosheni. Vijumba visivyofika 1000 vingewatoshaje wamasai Laki moja?

Baadhi ya video za wananchi wakiondoka kwenye eneo wanalotaka kumpa mwarabu wa OBC hizi hapa:

View attachment 2273617

View attachment 2273618

View attachment 2273651
 
SSH ni kiongozi makini sana. Huwa anaichukua ile mifupa inayowashinda viongozi wanaomtangulia halafu anaitafuna kwa umahiri wa hali ya juu.

Ni sawa na lile suala la kuhamisha wamachinga mitaani, likaonekana ni gumu sana lakini namna lilivyoshughulikiwa mpaka sasa hivi kumetulia kabisa.

Huu ndio uongozi unaotakiwa, akili na nguvu vinakuwa na uwiano ulio sawa.

..tatizo la serikali zetu ni KUKURUPUKA.

..hakuna mipango na mikakati ya muda mrefu. miaka mitano baadae usije ukashangaa kuna zoezi jipya la kuhamisha Wamaasai Loliondo.

..Tanapa na NCA ni mashirika yenye ukwasi mkubwa. Kwa maoni yangu walitakiwa wawe na mipango ya muda mrefu na shirikishi ya kudhibiti idadi ya watu na mifugo ktk maeneo yote ya mbuga za wanyama.

..Binafsi sijasikia kama kuna program ya Tanapa / NCA kuwafundisha na kuwawezesha Wamaasai kuwa wafugaji wa kisasa, na kuachana na asili ya kuchunga na kutembeza mifugo kwa malisho.
 
Tatizo kuu ni Wamasai kuondolewa katika eneo kwa lengo la kumpa mwarabu wa kampuni ya OBC aliyehonga watawala wetu toka enzi za mzee Ruksa ili apatiwe eneo hilo

Wamasai walipoondolewa Serengeti waliridhia na serengeti haikupewa mtu binafsi. Ila huko Loliondo watawala wanataka kumpa eneo hilo mwana wa mfame wa UAE afanye uwindaji.
Allegations za kumpa OBC hazina ulweli ni maneno ya kuwatia ndimu wananchi
 
Je ni kweli kuwa hizo kilomita za mraba 1500 ndizo anazopewa huyo mwarabu? mbona hilo hulisemei? Je hulisemei kwa bahati mbaya au
Mwarabu hajapewa hizo 1,500 km bali ana kitalu ambacho ana kodisha na kulipa ushuru toka mwaka 1992.
 
Back
Top Bottom