MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 32,408
- 50,809
Hehehe!! Lugha ya Kingereza huwababaisha na kuwatesa sana wenzetu wa kusini, yaani kitu cha kawaida kama rais kusoma hotuba iliyoandikwa kwa lugha ya kingereza anashangiliwa na kupongezwa sana, hamna anayejadili wala kutaja hoja za hotuba ya rais.
Watakuambia kingereza ni cha mkoloni hawakitaki mara Wachina hawajui kingereza lakini wanafanya makubwa, mara kingereza sio kipimo cha elimu, mara hiki mara kile, yaani vijisababu vyote vya kujiliwaza kwa kushindwa kujifunza kingereza.
Ukienda Bongo utakuta mabango kote yanatangaza nafasi za kujifunza na kuongea Kingereza ndani ya miezi mitatu, sijui nani kawadanganya lugha ni kitu cha kujifunza ndani ya muda mfupi hivyo na unaanza kutema yai moja kwa moja.
Watanzania wachache waliojifunza Kingereza na kukizungumza kwa weledi wananufaika pakubwa maana fursa zipo kibao, nyingi zinashikiliwa na wageni. Kila Mtanzania mwenye hela yake huhakikisha wanae wanasomea kwenye shule zinazofundisha kingereza, walalahoi wa st kayumba aka kajamba ndio wameachwa wakidangaywa wagande kwenye kiswahili tu eti ndio kujikomboa kutoka kwa wakoloni halafu nafasi za ajira zinapotangazwa humo wanachomekea "lazima ujue kuandika na kuongea kingereza kwa ufahasa"