Dawa ni kuboresha, mishara mazingira, nafasi za biashara na kazi Tanzania.
Hivyo vitu ni vigumu kuisha au kuidhibiti nchi nyingine.
Hapana swala ni maadili. Taifa kama China, walitumia miaka mingi sana kufundisha discipline kwa kizazi chao ili wawe na vizazi kama viwili vya watu wenye discipline ya kuchapa Kazi na kutengeneza thamani kupitia uzalishaji.
Matendo kama rushwa, uvivu, uzembe, uonevu, unyonyaji, dharau, na kadhalika huwa yalipewa adhabu kali sana ambazo katika dunia ya leo tutakimbilia kusema ni kinyume na haki za binadamu. Yote ilifanyika ili kujenga spirit ya watu ambao watasimamia malengo marefu ya vizazi vijavyo na kujenga taifa lao.
Ndio maana China miaka ya 1960 walikuwa kama sisi kiuchumi na hawakuwa mbali na sisi. Ila ndani ya hii miaka wamewekeza katika discipline na waliacha siasa za mazoea na za kuigaiga mataifa mengine na wameweza leo kujenga spirit ya uchapaji kazi leo china ina raia very sharp na wachapakazi tena wenye usongo sana wa maendeleo na hawawendekezi uzembe kwenye taifa lao.
Sisi hapa watu wanaiba mabilioni ya pesa tunawatetea waliwekwa ndani.
Watu wanafuja mali ya uma, wanahujumu miundo mbinu wanaiibia serikali na jamii sisi tunacheka tu na sheria zipo butu.
Watoto wanaishi wanavyotaka na wazazi hawana time. Wanawake na wanaume hawana malengo ya pamoja ni mashindano tu ya kipumbavu.
Wanawake wanawawaona wanaume wa taifa lao ni maadui zao na hivyo hawapo tayari kuwatii ila akija mzungu hata kama ni kapuku mwanamke wa kitanzania atamtii kwa adabu zote.
Hayo mambo machache ndio yanatengeneza kizazi cha namna hii ambacho hakina utetezi katika jamii yake na kuishia kudhalilishwa namna hii.
Unadhani angekuwa ni binti wa uingereza au raia wa kimarekani tena mzungu hiyo video ingeachwa, kwanza hao jamaa wangetafutwa kwa kila namna na wangewajibishwa.