Precious Diamond
JF-Expert Member
- Jun 9, 2023
- 593
- 1,376
Wananchi wa leo si kama wa wazamani, japokuwa kuna machawa wengi na wapumbavu wanotetea ujinga ili tu wapate V8 na kupanda ndege first class, wapo wanaojitambua, hata wale waliokuwa hawaelewi taratibu wanajielimisha na kusimamia haki zao.
Baada ya onyo hili kali lililotolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani Hamadi Masauni akiwa akizungumza na wanachama wa CCM Tawi la Kikwajuni Jimbo la Kinondoni jana tar 9/8/2023 kuwaambia wananchi wajiangalie wanapotoa maoni na kutoa agizo kwa Jeshi la polisi kuwachukulia hatua kali watu wanaohatarisha 'usalama wa taifa', wananchi wamesimamia vizuri uhuru wao wa kujieleza uliohakikishwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Toka tamko hilo litoke Watanzania masimama kidete, kiasi kwamba video hiyo imeondolewa YouTube, na hata baadhi ya vyombo vya habari vilivyokuwa vimerekodi tamko hilo pia kuliondoa kwenye vyombo vyao. Naona Azam wamejisahau tu, na wenyewe wangelishusha fasta.
Serikali, badala ya kuzuia watu kutoa maoni yao na kuwapangia vitu vya kuongea, wanatakiwa kulinda watu kutoa maoni yao bila hofu na kuwa tayari kupokea maoni na kurekebisha pale wanapokosea ili nchi iende vizuri. Kukataa kukosolewa kwa jina la 'Usalama kulinda Usalama wa Taifa' ni kunyima wananchi haki yao ya msingi na uhuru wao wao wa kujieleza
Ngoja tuweke kumbukumbu kwa vitabu vyetu ya aina ya viongozi tulionao.