POTOSHI Video ya moto kuhusu makao makuu ya IRGC nchini Iran

POTOSHI Video ya moto kuhusu makao makuu ya IRGC nchini Iran

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1

1784120521649.png
 
Tunachokijua
Madai

Video inayosambazwa mtandaoni inaonesha makao makuu ya Jeshi la Iran (IRGC) yaliyopo Tehran yakiteketea kwa moto baada ya kushambuliwa na Marekani.

Uhalisia

Ufuatiliaji wa JamiiCheck umebaini kuwa madai hayo si ya kweli. Kupitia reverse image search umebaini taarifa ya Reuters ya Novemba 26, 2025, inayoonesha tukio hilo likiwa ni moto mkubwa ulioteketeza majengo ya makazi ya Hung Fuk Court, Tai Po, Hong Kong. Video hiyo pia ilichapishwa na chombo cha habari cha Hong Kong, InMediaHK, kikieleza kuwa moto huo ulienea katika majengo kadhaa na kusababisha milipuko pamoja na miali mikubwa ya moto.

Aidha, vyombo mbalimbali vya habari viliripoti tukio hilo mwezi Novemba 2025, vikithibitisha kuwa video hiyo inahusiana na ajali ya moto kutoka Hong Kong na si mashambulizi dhidi ya makao makuu ya IRGC nchini Iran. rejea hapa na hapa.

Hivyo video inayodaiwa kuonesha makao makuu ya IRGC nchini Iran yakiteketea baada ya mashambulizi ya Marekani imepotoshwa. Kiuhalisia, inaonesha moto mkubwa uliotokea katika majengo ya makazi ya Hung Fuk Court huko Hong Kong mwezi Novemba 2025.​
Kwa viburi vyao wataisha wote.
Hivi ni ngumu kiasi gani kukubali kuwa aina Yako ya uongozi haifanyi kazi dunia ya Leo na ukaweka mambo fresh tu wananchi wako wakaishi pamoja na Dunia na ku'flourish vizuri tu?
 
Iran ni mwamba. Why? Kama mpaka leo anaweza kurusha chochote dhidi ya USA, basi ni Mwamba Si wa kudharai as you are portraying him...
 
Mpaka zinaletwa picha za uongo , USA hana makombora ya hivyo ..Hiyo ni apartments za pale Hong kong zilizoungua na moto 😀 😀
 
Iran ni mwamba. Why? Kama mpaka leo anaweza kurusha chochote dhidi ya USA, basi ni Mwamba Si wa kudharai as you are portraying him...

Mwamba sana ndo Taifa kubwa kwa sasa duniani
 
Vita sio vya kufurahia jamani , wamama na watoto na wazee wanateseka sana huko.
 
Hapo kagusa , hana makombora ya ajabu , tena karusha zaidi ya moja ..Kiufupi hana cha ajabu , endelea kutfauta picha fake
Mwisho jihadists mtasema kwamba hata Ayatollah hajafa ila bado anawalia gepu Marekani na Israel kwenye handaki moja isiyojulikana nchini Iran.

Ama kweli dini inalewesha kushinda bangi, nawashangaa wanaopiga bangi marufuku na kuacha dini ikiharibu akili za watu hasa waafrika.
 
Hakuna sehemu nimesema hivyo, wala sielewi umetokea wapi😅😅
 
Back
Top Bottom