Habarini wanajamvi,
Kama inavo jieleza hapo juu, hiyo video imesambazwa ikiwa na lengo kuu la kuleta mkanganyiko. Kama jadi ya wabongo kusambaza vitu visivyo na tija wala maana kwenye jamii.
Ukifatilia kwa makini utagundua Video hiyo lengo kuu ni kupotosha na hata ivyo aliyehusika sio yeye na hata hawafananii. Ifike mahali tukemee video kama hizi ambazo zinaharibu na kuchafua majina na nguvu kazi za taifaa.
Sijui ni kwanini inapofikia kwenye swala la video za utupu watanzania kwa ujumla wanakua na muemko kuliko kufatilia mambo ya msingi ambayo yanaweza kuwa na faida kwao, familia na taifa kwa ujumla.
Connection sio chakula wala haiongezi kipato tusishiriki kusambaza udhalilishaji huo.
NB: Nimezingatia kauli ya muhusika Meena Ally ambaye amekiri kuwa hajahusika katika video hiyo.