Video ya ng'ombe, Pundamilia na Binadamu Ngorongoro itufundishe Maasai wana haki ya kuishi

Video ya ng'ombe, Pundamilia na Binadamu Ngorongoro itufundishe Maasai wana haki ya kuishi

Kuna mawili either wanyama wahamishwe ili kulinda uhai wao ama wamasai wahamishwe, sasa kazi kwenu kuchagua ni lipi lenye unafuu maana ukisema uangalie historia tunaambiwa Hifadhi imewakuta wamasai hapo, basi ikiwezekana ifadhi ihamishwe Longido na wamasai wapewe Ngorongoro waendelee kuishi. Lakini nawaambia hao wanyama ni viumbe wa Mungu hawana wa kuwatetea wao wanajua kuishi na kufa tu. Ila wamasai wana utashi, wanaweza kuelimishwa ama hata kuhamishwa sehemu zingine na wakendelea na shughuli zao za kila siku. Tuache siasa kwenye mambo ya msingi kama Haya. Hii hifadhi sio ya wamasai pekee ni ya watanzania wote. Maslahi ya wanyama pia yazingatiwe
 
Kama watu wanaishi na wanyama wanaishi basi waache waishi tuu
 
Nani kakwamnia familia nyingi za kimasai hazijasomesha watoto mpaka chuo kikuu.? Mnaishi wapi ninyi? Lubega zivaliwazo zisikuchanganye, kuna kujielewa huku kusikomithilika.
Nazungumzia fani ya mifugo Mkuu. Pitia Tena andiko langu.

Kuna ndugu yangu alisoma kilimo. Alibadili sana mbinu za namna Bora za kuzalisha mazao mengi kwenye Eneo dogo.
 
Kuna ndugu yangu alisoma kilimo. Alibadili sana mbinu za namna Bora za kuzalisha mazao mengi kwenye Eneo dogo.
Inasemekana watanzania wa kimasai wamepeleka watoto wao wengi sana Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine.
 
Inasemekana watanzania wa kimasai wamepeleka watoto wao wengi sana Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine.
Hao Vijana Wakihitimu hapo wanapaswa kupangiwa Kazi Mpanda ,Songea, Mtwara n.k.
Watajikuta TU wanalazimika kuoa mke mmoja , watoto Wawili watatu au wanne.

Waafrika wote tuliishi maisha ya kuchanganyika na wanyama lakini maisha yanabadilika na kubadilika Kwa tabia nchi pia.
 
Siku moja nilipita Seronera kwa mbele nikaona kundi kubwa la simba ajabu hatua chache mbele nikaona wamasai watatu wana fimbo zao mgondoni wanapita eneo hilo bila kuwa na wasiwasi mbele.kwenda mbele zaidi nikakuta mtoto wa kimasai anachunga ng'ombe.
Ndani ya gari tulikaa na mmasai mmoja akatuambia ukishuka wewe Simba anakukamata lakini akiona mmasai anachanja mbuga sababu anaogopa atapigwa mshale akasema wewe Simba kamata wewe sababu umeogea sabuni na perfume sabuni lakini masai yeye napaka lukaria simba hapana kamata yeye naogopa.Kwenda tena mbele nikaona boma la wamasai nikaona wanachunga ng'ombe na pundamilia akatuambia wakati wa jioni ng'ombe wakirudi kwenye mazizi yao wanaandamana na pundamilia sababu pundamilia anajua akiwa na ng'ombe simba hawezi kuwasogelea.Hayo ndio maajabu ya wamasai kwa mawazo yangu wamasai ni moja ya watu wanasaidia kutunza wanyama hao maana kwa asili mmasai ni zambi kubwa kula nyama ya porini kwao ni tusi kubwa sana kula nyama za porini.Waachwe wamasai waishi kwenye mbuga na wanyama musiingize siasa.
 
Back
Top Bottom