Video ya Polisi akimshambulia kwa risasi kijana wa miaka 13 yatolewa Chicago

Video ya Polisi akimshambulia kwa risasi kijana wa miaka 13 yatolewa Chicago

Shadow7

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2020
Posts
24,606
Reaction score
39,289
Polisi wa Chicago wametoa picha za afisa aliyempiga risasi mtoto wa miaka 13 kwenye uchochoro wa giza.
118080634_269b0e87-bf10-4568-ba27-c18ba9b48cb9.jpeg

Video hiyo inaonesha polisi huyo akipiga kelele “dondosha” kabla ya kumpiga risasi Adam Toledo mara moja kifuani tarehe 29 mwezi Machi.
Mvulana haonekani kuwa ameshika silaha katika sekunde ya pili alipigwa risasi, lakini video ya polisi inaonesha bunduki karibu na mahali alipoangukia.
Maandamano madogo yalifanyika Alhamisi jioni karibu na Chicago, saa kadhaa baada ya meya wa jiji hilo kuomba utulivu.

Kutolewa kwa video hiyo kunafuatia tukio baya la polisi kufyatua risasi tarehe 11 Aprili dhidi Daunte Wright na afisa katika kitongoji cha Minneapolis.
Upigaji risasi huo umesababisha maandamano makali wakati jiji linasubiri matokeo ya kesi ya Derek Chauvin, afisa anayeshtakiwa kwa kifo cha George Floyd.

Video hiyo inaonesha nini?

Kipande hicho kinaonesha afisa huyo akiruka kutoka kwenye gari la kikosi chake na kumfukuza kijana huyo wa Latino kwa miguu chini kwenye uchochoro wenye giza wakati mtuhumiwa mwingine akipotea machoni.

Polisi huyo anapiga kelele: “Polisi! Simama! Simama sawa sasa hivi! Mikono! Mikono! Nioneshe mikono yako!”

Mvulana anageuka na kuinua mikono yake. Afisa anapiga kelele “Achia” na anapiga risasi – sekunde 19 baada ya kutoka kwenye gari la kikosi chake.
Picha tofauti za CCTV zinaonekana kuonesha kijana huyo akitupa kitu kwenye upenyo wa uzio wakati afisa huyo anamkimbilia. Video ya inaonesha maafisa wakimulika taa silaha nyuma ya uzio wa mbao baada ya ufyatuaji risasi.

Polisi huyo anaita gari la wagonjwa huku akimsihi kijana aliyeanguka “kuwa macho”. Maafisa wengine wanafika katika eneo hilo katika kitongoji cha Little Village upande wa magharibi mwa jiji na hatua ya kurejesha mapigo yake ya moyo (CPR) inafanywa.
Kulingana na waendesha mashtaka, kijana huyo alikuwa na mtu wa miaka 21, Ruben Roman, ambaye alikuwa amefyatua bunduki kwenye gari lililokuwa likipita. Milio ya risasi iliwavuta polisi katika eneo hilo, na kusababisha makabiliano makali.
Bwana Roman alijitokeza mahakamani Jumamosi akishtakiwa kwa utumiaji mbaya wa silaha, utapeli wa silaha na kuhatarisha maisha ya watoto, kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari.

Ofisi ya Uraia ya Uwajibikaji wa Polisi ilitoa picha za kamera siku ya Alhamisi pamoja na video ya CCTV, ripoti za kukamatwa na rekodi za sauti za risasi zilizopigwa katika eneo hilo ambalo liliwajulisha polisi.

Tukio hilo linazungumziwaje?​

Muda mfupi kabla ya video hiyo kutolewa, Meya wa Chicago Lori Lightfoot alifanya mkutano na waandishi wa habari ambapo aliita video hiyo “ya kuumiza” kutazama.

“Kwa kifupi, tulikosea kwa Adam,” alisema. “Na hatuwezi kumudu kufanya makosa kwa kijana mwingine katika jiji letu.”
Meya Lightfoot aliwahimiza umma kubaki watulivu
Meya wa Chicago Lori Lightfoot

“Tunaishi katika jiji ambalo linaumizwa na historia ndefu ya vurugu za polisi na utovu wa nidhamu,” meya huyo alisema. “Kwa hivyo wakati hatuna habari za kutosha kushutumu kuhusu hili, inaeleweka kwa nini wakazi wetu wengi wanahisi kuongezeka kwa hasira na maumivu.”
Familia ya Toledo pia imeomba watu kuwa watulivu.

“Tumesikia ripoti kwenye vyombo vya habari kwamba maandamano zaidi yamepangwa leo, na wakati hatuna ufahamu wa moja kwa moja wa matukio hayo, tunaomba kwamba kwa ajili ya jiji letu, watu wabaki na amani kuheshimu kumbukumbu ya Adam na kufanya kazi nzuri kuchochea mageuzi “walisema katika taarifa yao.

Kwenye mkutano na waandishi wa habari Alhamisi, wakili wa familia ya Toledo Adeena Weiss Ortiz alisema kuwa kijana huyo hakuwa ameshika bunduki wakati alipopigwa risasi.

Lakini alisema hawawezi kusema kwa “uhakika wa 100%” ikiwa kijana huyo alikuwa amebeba silaha kabla ya tukio hilo , gazeti la Chicago Tribune liliripoti.
Afisa aliyefyatua risasi hajatuhumiwa rasmi kwa makosa. Anasubiri matokeo ya uchunguzi ikiwa alifuata utaratibu mzuri wa matumizi ya nguvu.
Ana miaka 34 aliyejiunga na jeshi mwaka 2015 na hana rekodi ya malalamiko, kulingana na Chicago Sun-Times.

 
Back
Top Bottom