PostGE2025 Video: Yaliyofanyika si maandamano ni uharibifu, jaribio la mapinduzi ni tafsiri ya UGAIDI

PostGE2025 Video: Yaliyofanyika si maandamano ni uharibifu, jaribio la mapinduzi ni tafsiri ya UGAIDI

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Uko nje kabisa na nilichouliza. Sijazungumzia maandamano popote katika bandiko langu.
Lisome tena.
Hukujibu maswali yangu uliukiza pia lait ungekitoa majibu ningelitoa pia jibu.

Kumbuka pande zote mbili lazima zikiri ili kusonga mbele
 
Wewe umeeleza kuhusu uharibifu uliofanywa na raia👇
Je barabara hazikufungwa?? Vituo vya mafuta havikuchomwa?? Maduka hayakuvunjwa?? Je mawe hayakurushwa kwa wasio na hatia?? Je vituo vya kupigia kura havikuchomwa???
Swali; Hakuna njia nyingine ya kupambana na raia wanaofaya hayo uliyoorodhesha hapo tofauti na kuwapiga risasi kama nyani??
 
Jamaa walifeli sana, kinachosikitisha wanatumia nguvu nyingi kujetetea.
 
Wakuu nimekutana na andiko hili...

Ni nani aliwapa ujasiri wa kuchoma mali za watu wasio na hatia?Ni nani aliwapa moyo mgumu kiasi cha kufunga barabara ambazo hata mgonjwa aliyehangaika na pumzi yake ya mwisho alipitia? 🚑

Mamilioni ya jasho ya mtu mmoja yaligeuzwa majivu ndani ya dakika chache. Mama aliyekuwa anategemea duka lake ili kuwalisha watoto wake, leo amebaki na machozi tu.Kijana aliyekuwa anategemea pikipiki yake kujihifadhi na kulipa kodi ya maisha, leo amebaki hana chochote. 😔

Na kibaya zaidi… Hawa waliokuwa wanaita eti mapambano, hawakuwa na huruma, hawakuwa na lengo la kujenga, walitaka kuharibu. Walileta hofu, uvunjifu wa amani, na maumivu makali kwa watu wasiostahili.

Watu kama nyie ndio mnaosababisha machawa wanachomewa ndani ya nyumba.
 
Back
Top Bottom