OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Napata shida sana kuangalia clips za marudio ya hii match. Napata shida kuona mpira ukichezwa kama vita na ugomvi. Najiuliza faida ya rafu hizi ni nini. Mbali na upinzani wa timu lakini wachezaji hawa ni washikaji na wote wanapigania uzima ili kujenga maisha yao. Sasa inakuwaje jitu linacheza rafu ya kiwango hiki bila kujali usalama wa wengine?
Zaidi najiuliza ni nani anawafundisha kufanya haya?haya yanaweza kuwa maelekezo ya mwalimu?
Hii timu sio ya kuombea mafanikio kabisa