Digaller
JF-Expert Member
- Oct 20, 2009
- 798
- 541
angekua ni kiungo cha ubishi gentleman,
Rais ameshatoa maagizo na maelekezo muhimu sana kwa kamati ya maafa Kitaifa kama ambavyo pia hufanya vivyo hivyo kwenye ajali na maafa mengineyo nchini.
Kumbuka,
Kamati ya maafa Kitaifa inaongozwa na Kasimu Majaliwa, waziri Mkuu ambae yuko field kupitia vyombo vya ulinzi na usalama..
huku kazi ya uokozi ambayo inafanyika kwa umakini mkubwa ikiendelea kufanyika kwa weledi na bidii sana.
Mola atujaalie subra na wepesi katika kufikia hitimisho jema juu ya jambo hili.
Vyovyote itakavyokua, kama Taifa lazima tusonge mbele pamoja 🐒
Onyesha busara zako kwa kuficha upumbavu wako, angekuwa aliekufa ni Mohamed Mchengerwa unadhani Samia angesafiri?
Ila kwakuwa maisha ya watanzania wapambanaji sio muhimu kwake ndio maana anaweza kuondoka huku akiacha nyumba yake inateketea.
Waliopo karibu na raisi hawamsaidii hata kidogo, ni kitu kidogo sana, ni kumwambia ukweli kuwa si jambo la busara kuondoka huku watanzania wenzake wamekwama kwenye kifusi na wanapambania maisha yao.
Hata huku mtaani huwa tunaomba ruhusa kazini pale mwenzetu anapopatwa na msiba ili tukashiriki pamoja nae na ndio utanzania ulivyo.
Sote njia yetu ni moja, hakuna haja ya kubaguana.