Video za uokozi maafa ya kariakoo


Onyesha busara zako kwa kuficha upumbavu wako, angekuwa aliekufa ni Mohamed Mchengerwa unadhani Samia angesafiri?

Ila kwakuwa maisha ya watanzania wapambanaji sio muhimu kwake ndio maana anaweza kuondoka huku akiacha nyumba yake inateketea.

Waliopo karibu na raisi hawamsaidii hata kidogo, ni kitu kidogo sana, ni kumwambia ukweli kuwa si jambo la busara kuondoka huku watanzania wenzake wamekwama kwenye kifusi na wanapambania maisha yao.

Hata huku mtaani huwa tunaomba ruhusa kazini pale mwenzetu anapopatwa na msiba ili tukashiriki pamoja nae na ndio utanzania ulivyo.

Sote njia yetu ni moja, hakuna haja ya kubaguana.
 
Sawa wasalimie huko Sao Paulo na Acapulco bay.
 
Gentleman,
hata wewe kipara chako chenye ukaidi wa kinyumbu si kwenye avatar tu lakini mtaani ni full mvi, right?🐒
Nenda pale kwenye uokozi ulete huo uchawa wako, hakyanani unaliwa mande kijana, nyie toeni pongezi humuhumu na kwenye mikutano yenu ile ya kipigaji ama lah jihakikishie ulinzi kabla hujaropoka uharo.
 
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji CGF John Masunga, amesema bado kuna mawasiliano kati ya Jeshi hilo na Watu walionasa chini ya jengo la ghorofa lililoporomoka Kariakoo jijini Dar es salaam.

CGF Masunga ameyasema hayo mbele ya Waandishi wa Habari asubuhi hii ambapo pamoja na kufanikiwa kuwapatia hewa ya oxygen, amesema tayari wamewapelekea Watu hao maji pamoja na glucose.

“Bado kuna Watu wako chini na mawasiliano yanafanyika na Watu hao ni wazima, tumefanikiwa kuwapatia maji, glucose pamoja na kuwapa faraja kwamba Vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama vipo hapa na tutahakikisha wanatoka wakiwa wazima, tumefarijika sana kwasababu tumeweza kuwapatia hizo huduma wakiwa ndani ya shimo lakini pia tumeweza kuwasiliana nao, huduma ya uokoaji inaendelea”

“Mpaka sasa Majeruhi kadhaa wameendelea kupatikana kutoka kwenye basement ya jengo na wamepelekwa Hospitali kwa ajili ya huduma, Vikosi vya Uokoaji vipo imara kuhakikisha kwamba Ndugu zetu waliochini kwenye kifusi wanapatikana wakiwa salama, tuna vifaa vya kutosha...” ——— CGF John Masunga. #MillardAyoUPDATES
 
HEwa na faraja ndio jambo la msingi
 
Hivi unataka nini??? Pumbavu kabisa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…