Video za uokozi maafa ya kariakoo

Mguu wangu umebwa na kitu kama jabali zito, nashindwa kabisa kujinasua hapa, tangu asubuhi nimelala, siwezi kugeuka, nahisi, kuchoka, maumivu hayaelezeki labda nimevunjika, maana mguu unauma sana. Mwili unakosa nguvu.

"Dalili za uhai ni ndogo kuliko kifo
mbaya zaidi nakufa taratibu, kwa maumivu makali...nimechoka sana, najisikia vibaya, nashikwa na kichefu chefu, nikivuta pumzi, navuta vumbi inayonipa kikohozi. Joto ni Kali na hewa ni nzito sana.

Nakufa Mimi, tena nikiwa masikini Ally.

Awali nilidhani muda si mrefunitaokolewa lakini Sioni dalili zozote za kufikiwa, nakufa Mimi jama, nikiwa Sina chochote nilicho acha kwa ajili ya watoto wangu.

Msaidieni mama Yasir, wasaidieni watoto wangu, wasaidieni tafadhali. Fanya kwa ajili yangu kama nitakufa....

Mwambia mama Yasir nampenda sana, Nilipambana Kwa ajili ya familia, anajua hilo .ila jitihada hazishindi kudra.
 
Unamjua Edward?
 
Kama kuna mtu ana ndugu, rafiki au mdau yeyote yuko chini ya kifusi kariakoo mambo ya kuzingania kwa sasa ni haya

—- Waambiee wapunguze harakati huko chini ili kulinda kiwango cha Oxygen wanachotumia na energy, unless kama uko sure hiyo harakati itamtoa huko chini kama hana matokeo hayo ni bora wakatunza Oxygen ya eneo walilopa kwa kutofanya movement, kwa maana nyingine watulie hili mwili usitumie energy waliyonayo na kuitaji hewa pia

— Mbili wazime simu kwa sasa ili kukoa chache ila watoe taarifa walikuwa floor ya ngapi kabla ya jengo kuanguka , simu ziwashwe kesho kama wakipata dharura ndio wawashe kutoa taarifa pia waangalie bandle na kutumiwa kama linakaribia kuisha

Mwisho, kwa ndugu waliopo nje kesho anzieni kwa Chalamila ikiwezekana mkabeni masharti awajibu thamani ya ndugu zenu ni kiasi gani kwake
 
Nchi hii tumewahi kupata viongozi wawili Tu wanaoguswa na madhila ya maskini, Hayati Ali H. Mwinyi & John P. Magufuli, Mwenyenzi Mungu awarehemu.

The rest ni majanga tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…