Mh. Lema amesema kwa amemsoma sana Mandela alipokuwa gerezani,Katika kitabu chake cha Long walk to freedom na amesema ilikuwa bahati alipata muda wa kukimaliza kitabu hicho.
Anasema kinachomstua zaidi kwenye hali ya sasa pamoja na mfumo wa vyama vingi uliopo kwa sasa ambayo inatekeleza demokrasia na utawala bora
Amesema ukiona viongozi wanaishu wanavyotaka bunge linaamua linavyotaka mahakama inaaanza kutumia maoni yake kuamua na sio kwa mujibu wa sheria bali ni kwa maoni ya hakimu.
Amesema kuwa kama kmwananchi wa kawaida hawezi kuona uchungu mbunge kwenda jela kwa uonevu hawezi kuona uchungu kama mwananchi mwenzake akienda jela kwa uonevu ameongeza kuwa ni wakati wa kulifanya taifa lione kuwa mtu akienda jela kwa uonevu sio sahihi na aone uchungu kama ndugu yake wa karibu ndio ameonewa.
Pia mh. Joseph Mbilinyi amesema kuwa kufungwa kwao wao ni mwanga wa kuwa serikali iliopo madarakani haina sera ila sera yao ni kuzalisha wafungwa wa kisiasa yaani serikali ya fungafunga.
Amesema kuwa kwa upande wake yeye haelewi wanyonge ni kina nani kama jinsi serikali iliyopo madarakani inavyojinasibu kuwa ni serikali ya wanyonge ameongeza kuwa huenda wale wanaopiga makofi kwa serikali ndio wanyonge maana kama ni serikali ya wanyonge ni ajabu kuona wanyonge wanaotetewa wanapanga foleni kununua sukari.
Amesema kuwa ukiona kila unachokifanya kinadidimiza haki basi wewe ni dhaifu kwa kuwa alie dhaifu si yule anae onewa bali ni yule anae onea kwani kwa kuwa ni dhaifu basi silaha yake ni kuonea ili kuficha udhaifu alionao.
Mh. lema amesema kuwa hakuna kitu kina thamani kuliko haki na ndio maana hawezi kuuza haki kwa sababu ya pesa na wala hapangi anashundaje Arusha ila anajua atashunda Arusha, na wala hawezi kushunda kwa kuuza haki kwa au vinginevyo.
Amesema kuwa walipoamua kujiweka karantini ilikuwa ni kutuma ujumbe kwa serikali kuwa corona io na ni hatari na pia kuweza kujiangalia wao kama wako salama na kuihimiza serikali iweze kuongeza hatua zaidi kwenye mapambano dhidi ya corona na ndio maana walikuwa tayari kupoteza posho zao.