GE2025 Videos: Vurugu za wanaCCM kwenye zoezi la uteuzi wa wagombea ubunge sehemu mbalimbali nchini

GE2025 Videos: Vurugu za wanaCCM kwenye zoezi la uteuzi wa wagombea ubunge sehemu mbalimbali nchini

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
JE MASHETANI WAINGIA KUPIGA KURA CCM?

Kwa mujibu wa Msimamizi wa Uchaguzi katika Jimbo moja huko Kaskazini, Idadi ya wapiga kura ilikiwa ni 1252, kura zilizoharibika ni 7 kwa hiyo jumla ya kura halali ni 1245.

Jumla ya matokeo ya kura zilizotangazwa ni (9+50+95+141+196+213+775+1004) ambapo hesabu hii inatupa jumla ya kura 2483. Hivyo Msimamizi wa Uchaguzi ametangaza juma ya kura 2483 ambapo zimeongezeka kura hewa 1238. Hii ina maana ya kuwa kulikuwa na kura hewa zenye idadi sawa na idadi ya wajumbe wote ambao walikuwa ukumbini kupiga kura.

'Mlevi wa Itigi' huku kitaani amesikika akisema "Hiyo ni ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM).
Sisi tukisema hakuna mifumo ya haki hawataki. Taifa hili linahitaji mabadiliko kwenye mifumo yote ya uchaguzi. Na kama CCM wenyewe kwa wenyewe wanafanyiana mambo hayo, je kama wakiwa na ulinzi wao wa Polisi watawafanyiaje wapinzani"?

Lakini Hoja ya 'mlevi' huyo imetufikirisha sana kwani inaonekana ana akili kuwazidi wajumbe wote wa CCM 1252 waliokuwepo ukumbini na hasa ikizingatiwa ya kuwa hakuna aliyehoji juu ya hizi kura za mashetani ambazo zilitangazwa na Msimamizi wa Uchaguzi. Je, zilitoka wapi? Je, kama CCM imeshindwa kuweka Tume Huru ya Uchaguzi kuendesha chaguzi ndani ya CCM, itawezaje kuweka Tume Huru ya Uchaguzi kwa ajili ya kusimamia Uchaguzi Mkuu wa kitaifa?

Huyu Msimamizi wa Uchaguzi hakuwa na haja ya kujumlisha kura wala hakuwa na mamlaka kamili na uchaguzi huo! Huo ndio uhuni sasa!
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Itunge, Dar es Salaam; 5 Agosti 2025; saa 6:15 usiku.

View: https://www.facebook.com/share/v/16zSicCJQW/?mibextid=D5vuiz
 
✂️Kule Nzega vijijini Dr Hamis Kigwangala wajumbe wamemnyoa ,shwaaaaaa✂️
FB_IMG_1754349528824.jpg
 
Mtia nia wa Ubunge katika Jimbo la Iringa Mjini, Fadhili Ngajilo amewashinda wapinzani wake katika kura za maoni za Chama cha Mapinduzi (CCM) jimboni humo akipata kura 1899 huku Moses Ambindwile akipata kura 1523,Peter Msigwa kura 477, Jesca Msambatavangu kura 408, Islam Huwelii kura 136, N...

View: https://www.facebook.com/share/v/1Hhv8K1fbY/
 
Dhambi ya usaliti. Huyu Mchungaji laana ya usaliti inamtafuna. Namshauri arudi madhabahuni afanye huduma za kiroho aachane na siasa
 
Back
Top Bottom