SoC02 Vidole vya mkono wangu siri ya mafanikio yangu

Stories of Change - 2022 Competition

Rupia Marko D

Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
39
Reaction score
63
Ndipo nilipokaa chini pembezoni kidogo na ukingo wa kitanda changu nikiwa nimegubikwa na shauku kubwa ya mafanikio. Kama Kijana mdogo nijuaye kwa hakika na dhairi shairi kua Maisha haya ni duara, hivyo nisimame imara kuligombania Kombe na kuanzisha safari yangu ya Mafanikio. Nikijua kwamba kama Kijana katika mali za wazee wangu mimi sina changu.

Na hivyo kama naitaka mali lazima niingie shambani ili kuichuma na kamwe ni siwe kama yule sungura aliyesema, sizitaki hizi mbichi na kukataa tamaa. Na hivyo nichukue Mundu na kuingia mgodini, kuitafuta dhahabu ya Mafanikio na katika safari hii ndefu na nyembamba, lazima niongozwe na Falsafa na Sheria yangu, itakayoniongoza ambayo pia ya weza kuwaongoza vijana wenzangu kama mimi iwe taa katika Mafanikio yetu.

Basi nikaona katika yote ninavyo vidole vitano katika mkono wangu, basi sio mbaya kuwa nivitumie hivi kama mwongozo na Falsafa itayoniongoza na kutuongoza sote katika safari hii ndefu.

KIDOLE GUMBA
Basi nikaona katika kidole hiki, kuwa cha simama badala ya Nguvu, ujasiri, uthubutu,umaridadi, ujuzi na ueredi. Kiashiria kidogo kua cha simama badala ya nguvu waweza kutazama katika masumbwi, kuwa wanamasumbwi huimarisha ngumi zao kwa kidole hiki. Pia wasomi hutumia kidole hiki kuzibana karamu zao ili kuandika mambo wayatakayo.
Ikumbukwe pia Mwl.Nyerere mwaka 1978 alitumia Falsafa ya kidole hiki kumpiga nduli Iddi Amin Dada aliposema "Uwezo wa kumpiga tunao . Sababu ya kumpiga tunayo, na Nia ya kumpiga tunayo. Tunataka dunia ituelewe hivyo. Kwamba hatuna kazi nyingine ( Hotuba ya Mwl. Nyerere mwaka 1978).Na kweli tulifanikiwa.
Hivyo tuone katika kidole hiki Nguvu, ujasiri, kujiamini,uthabiti,ueredi na ujuzi hivi vitu vyaweza kua taa katika safari hii.

KIDOLE CHA SHAHADA
kidole hiki chasimama kama mtazamo,ndoto,upeo na hatima. Mfano tu rahisi akija mtu umwelekeze uelekeo fulani, tunatumia kidole hiki kumwelekeza na kusema "sehemu fulani ni pale"
Kidole hiki kitufanye kuona katika ndoto zetu, kama unandoto ya kua mwalimu basi ona tayari upo mbele ya darasa ukifundisha hata kama bado hujawa mwalimu, kama unandoto ya kuwa daktari ona tayari ukimhudumia mgonjwa,kama unandoto ya kua Mwimbaji mkubwa ona tayari upo katika jukwaa kubwa ukitumbuiza na mengine mengi kama haya.

KIDOLE CHA KATI
Kwa muonekano tu kidole hiki chaonekana kuwa kirefu kuzidi vyote, urefu huu wawakilisha nini?
Urefu huu unawakilisha upekee, Je ni upekee gani huo?
Upekee huu ni katika uwajibikaji wetu wa kila siku, lazima tuwe na kitu ambacho chaweza tutofautisha na wengine ili kwamba kwa kitu hicho hata tukisimama katika kundi kubwa tuweze kuoneka. Mfano:-Ukianzisha biashara sehemu yenye maduka mengi lazima uchunguze kitu gani ambacho jirani yako hana kwa kufanya hivyo mteja akija akikosa kwa jirani akipate kwako na hivyo biashara yako itakua juu kabisa kama kidole hiki. Kidole hiki kitafunye tuwe na uwezo wa kuonekana hata katika kundi kubwa la watu, na watu hao watuone kwani mafanikio yetu yapo katika watu.

KIDOLE CHA PETE
Kidole hiki chasimama badala ya kujitoa (commitment),hii inamaana ya kuwa radhi na matokeo yoyote yale, utayari wa kufanya jambo hata kama jambo hilo likiwa na vikwazo vikubwa.
Pia kuwa na ile hali ya kujisemea ndani ya nafsi yako maneno ya kukupa ujasiri na Nguvu, kama kurudia kila mara kujisemea katika nafsi kuwa "naweza", "uwezo ninao", "mimi ni bora". Ni maneno haya hupandisha morali wa kufanya kazi, kwani hata vitani wanajeshi hujitoa kufa na kupona kwa maneno ya kutia nguvu.
Na kama tujuavyo kidole hiki huitwa cha pete kwa sababu pete huvikwa katika kidole hiki utani husema "mshipa wa damu wa kidole hiki umeenda moja kwa moja hadi katika moyo"-hivyo mtu kuvaa pete katika kidole hiki humaanisha "nakupenda toka katika kilindi cha moyo wangu"
Hivyo kidole hiki kituonyeshe kua kwa kujitoa katika shuguli zetu ndipo palipo na mafanikio yetu yalipo.

KIDOLE KIDOGO
Kwa muonekano wake tu hata mtoto mdogo hukitambua kua ni kidole kidogo katika vyote. Je kwa udogo wa kidole hiki twachota falsafa gani?

licha ya udogo wake kidole hiki chatoa fundisho kubwa maishani, ndio msingi wa yotee katika mafanikio ya Mwanadamu, katika safari yake ya kila siku. Katika udogo wake kidole hiki chabeba ujumbe huu Katika Maisha yetu tusividharau vitu vidogo.

Kwanini tusiwe na dharau?
Hii ni kwa sababu haba na haba hujaza kibaba, sarafu ya shilingi hamsini ikitolea katika Noti ya Elfu kumi, Elfu kumi hua si kitu tena.

Hebu tazama kwa makini ukiingia karibu kila duka utakuta bidhaa ndogo ya Shilingi hamsini, hii ina maana kua licha ya utajiri mkubwa wa wamiliki viwanda na matajiri wakubwa huthamini hata bidhaa ndogo ili hali wakijua haba na haba hujaza kibaba, hamsini huunda Mia, Mia huunda mia tano, mia tano huunda elfu mmoja kutoka kwa hii elfu kumi na laki hupatikana.

Vijana wenzangu tukumbuke kua Roma na ukubwa wake ule haikujengwa kwa siku moja, ilijengwa kidogo kidogo siku moja tofali mia tano,kisha msingi, nguzo, ukuta na mwisho Roma yote ikamalizika.

Hivyo nasi safari yetu hii ya mafanikio tusiindeshe haraka haraka na kwa pupa, kwani wahenga walisema mtaka yote kwa pupa hukosa yote, vijana wenzangu hakuna utajiri wa haraka wenye kukaa mda mrefu hivyo tusiote ndoto za mchana na kujiingiza katika shuguli hatarishi kama kucheza kamari, tusije fanana na muuza kahawa aliyekua akitembeza kahawa zake kisha kuamua kupumzika chini ya mti na kupitiwa na njozi, na katika njozi hio kujiona Mfalme akiwa na vijakazi wengi kisha katika ndoto ile falme ile ikavamiwa kisha kuvamia akakurupushwa kwa kukoshwa na mkuki kwa papala Muuza kahawa akakurupuka na kuvunja chupa ya kahawa pamoja na vikombe vyake, Hivyo tuamke katika ndoto zetu za mchana zisije tutia katika wingu kubwa la umaskini.

Mwisho Vijana wenzangu si andiki kama mwanariadha aliye umaliza mwendo la hasha kama yule aliye katika kuanza, hivyo ni imani yangu kua haya mambo madogo yanaweza kua taa ya msingi katika mafanikio yetu.

ASANTENI SANA.
 
Upvote 25

Utafika mbali sana dogo
 
Unaweza
 
Back
Top Bottom