Kidagaa kimemwozea
JF-Expert Member
- Jul 13, 2018
- 3,680
- 6,554
Anayedaiwa kumiliki na kuendesha tovuti haramu ya kusambaza filamu maarufu ‘FMovies’ mapema mwezi uliopita alitambulishwa baada ya kukamatwa na Polisi wa Mji wa Hanoi nchini Vietnam kufuatia uchunguzi wa muda mrefu.
Phan Thanh Cong, 34, raia wa Vietnam aliyekamatwa na mshirika wake, Nguyen Tuan Anh, wanasemekana waliendesha tovuti hiyo na kujizolea ‘pesa nyingi’ kutokana na matangazo.
Hii ni kwa mujibu wa Torrentfreak, tovuti inayofuatilia habari za hakimiliki mtandaoni.
Tovuti ya Fmovies iliyofungwa na mamlaka ya Vietnam mwezi Julai 2024, ilihudumu tangu 2016 na inadaiwa kusambaza filamu na vipindi vya televisheni takriban 50,000 bila leseni kutoka kwa watayarishaji na wamiliki halali.
Kulingana na Motion Picture Association (MPA) na Alliance for Creativity and Entertainment (ACE), FMovies na tovuti zingine chini ya mwamvuli wake ndizo zilikuwa vyanzo vikubwa zaidi ulimwenguni vya usambazaji haramu wa filamu, ikivutia zaidi ya watumiaji bilioni 6.7.
Disemba mwaka 2023, Makamu wa Rais Mtendaji Mkuu wa Motion Picture Association (MPA), Karyn Temple, alifika mbele ya kamati ya bunge la Marekani, na kuonesha jinsi tovuti hiyo ilivyokuwa ikifanya kazi, akidai kuwa FMovies ilichangia kusababisha hasara ya dola bilioni 29.2 kwa mwaka katika sekta ya filamu ya Marekani maarufu Hollywood.
ACE na MPA ziliandikia barua Idara ya Polisi ya Hanoi kuwashukuru kwa kumkamata Cong, ambaye anatuhumiwa kwa makosa ya kukiuka hakimiliki.