Vietnam: Mmiliki wa Tovuti ya kusambaza Filamu haramu akamatwa

Sites zipo nyingi sana, wakifunga hii watu wanafungua nyengine. Ni vita ngumu sana kwao kuishinda.
 
Fmovies ina proxy nyingi sana hawawezi kuzizuia
 
Anayedaiwa kumiliki na kuendesha tovuti haramu ya kusambaza filamu maarufu ‘FMovies’ mapema mwezi uliopita alitambulishwa baada ya kukamatwa na Polisi wa Mji wa Hanoi nchini Vietnam kufuatia uchunguzi wa muda mrefu.

Phan Thanh Cong, 34, raia wa Vietnam aliyekamatwa na mshirika wake, Nguyen Tuan Anh, wanasemekana waliendesha tovuti hiyo na kujizolea ‘pesa nyingi’ kutokana na matangazo.

Hii ni kwa mujibu wa Torrentfreak, tovuti inayofuatilia habari za hakimiliki mtandaoni.

Tovuti ya Fmovies iliyofungwa na mamlaka ya Vietnam mwezi Julai 2024, ilihudumu tangu 2016 na inadaiwa kusambaza filamu na vipindi vya televisheni takriban 50,000 bila leseni kutoka kwa watayarishaji na wamiliki halali.

Kulingana na Motion Picture Association (MPA) na Alliance for Creativity and Entertainment (ACE), FMovies na tovuti zingine chini ya mwamvuli wake ndizo zilikuwa vyanzo vikubwa zaidi ulimwenguni vya usambazaji haramu wa filamu, ikivutia zaidi ya watumiaji bilioni 6.7.

Disemba mwaka 2023, Makamu wa Rais Mtendaji Mkuu wa Motion Picture Association (MPA), Karyn Temple, alifika mbele ya kamati ya bunge la Marekani, na kuonesha jinsi tovuti hiyo ilivyokuwa ikifanya kazi, akidai kuwa FMovies ilichangia kusababisha hasara ya dola bilioni 29.2 kwa mwaka katika sekta ya filamu ya Marekani maarufu Hollywood.

ACE na MPA ziliandikia barua Idara ya Polisi ya Hanoi kuwashukuru kwa kumkamata Cong, ambaye anatuhumiwa kwa makosa ya kukiuka hakimiliki.View attachment 3189597
Unaweza kuta hao polisi wenyewe pia walikua wanatumia fmovies
 
Anayedaiwa kumiliki na kuendesha tovuti haramu ya kusambaza filamu maarufu ‘FMovies’ mapema mwezi uliopita alitambulishwa baada ya kukamatwa na Polisi wa Mji wa Hanoi nchini Vietnam kufuatia uchunguzi wa muda mrefu.
Uandishi mzuri unataka title iwe clear! Kupitia title nilielewa kwamba movies zinazosambazwa na hiyo tovuti (FMovies) ni haramu kumbe kimsingi haramu sio movies bali tovuti ndio haramu kwa muktadha kwamba haifuati taratibu zinazotakiwa. Please, rephrase the heading.
 
Asilimia 100 ya watu duniani wanatumia free site hakuna downloading kupungua wanaongoza kuchakachua movie ni sie tuna download na hauwezi kuzuia uchakachuaji kwenye movie na series Dunia ya sasa ndio maana ili uweze kusambaza movie inatakiwa upate vibali kwa sasa ukipata hautapata tabu sana
Mkuu hebu nipe link za site ambazo watu asilimia 100 duniani wanadownload for free baada yakupata VIBALI kama walivyokua wanadownload kwenye FZmovies?

Mfano Tyler Perry katumia mamilioni ya dola kutengeneza movie ya The Six Triple Eight halafu wewe unakwenda kuomba kibali watu wadownload free?
The Six Triple Eight utaipata kihalali NETFLIX pekee

Siku hizi hakuna VIBALI vya biashara ya kudownload movies dunia imehamia kwenye streaming
Movie ukitoka akina Amazon, Hulu, Netflix, Appel Tv+ wanagombania kupata haki za kustream

Ukiona mahali popote pale unadownload movies for free basi ujue ni ama ni movies ambazo zipo bure au ni magendo (pirates)

So hakuna namna yoyote huyo mwamba wa FZmovies angeweza kupata vibali ku download movies free zaidi ya kufanya magendo
 
The Six Triple Eight utaipata NETFLIX pekee

Siku hizi hakuna VIBALI vya biashara ya kudownload dunia imehamia kwenye streaming

Ukiona mahali popote pale unadownload movies for free basi ujue ni ama ni movies ambazo zipo bure au ni magendo (pirates)

So hakuna namna yoyote huyo mwamba wa FZmovies angeweza kupata vibali ku download movies free zaidi ya kufanya magendo
Hicho kibali hakitolewi. Wanaposema hivyo wanamaanisha huruhusiwi ku sambaza otherwise uwe na kibali hapo nikama katazo , maana mtu au kampuni hawawezi kukupa kibali ilihali wao hawaingizi kitu huku wewe ukiingiza mabilion
 
Mkuu hebu nipe link za site ambazo watu asilimia 100 duniani wanadownload for free baada yakupata VIBALI kama walivyokua wanadownload kwenye FZmovies?

Mfano Tyler Perry katumia mamilioni ya dola kutengeneza movie ya The Six Triple Eight halafu wewe unakwenda kuomba kibali watu wadownload free?
The Six Triple Eight utaipata kihalali NETFLIX pekee

Siku hizi hakuna VIBALI vya biashara ya kudownload movies dunia imehamia kwenye streaming
Movie ukitoka akina Amazon, Hulu, Netflix, Appel Tv+ wanagombania kupata haki za kustream

Ukiona mahali popote pale unadownload movies for free basi ujue ni ama ni movies ambazo zipo bure au ni magendo (pirates)

So hakuna namna yoyote huyo mwamba wa FZmovies angeweza kupata vibali ku download movies free zaidi ya kufanya magendo
Piratesbays
Medeberiyaa
Goojara
Yts
Nkiri
Magnet dl
 
Hicho kibali hakitolewi. Wanaposema hivyo wanamaanisha huruhusiwi ku sambaza otherwise uwe na kibali hapo nikama katazo , maana mtu au kampuni hawawezi kukupa kibali ilihali wao hawaingizi kitu huku wewe ukiingiza mabilion
Ni kweli mkuu
 
Ndio mkuu ndio maana wamiliki wake hawafungwi
Mkuu hizo Site ulizozitaja hazina tofauti yoyote na FZmovies....... ni swala la muda tu

Site za wizi wa movies zipo nyingi lakini zinashughulikiwa kwa kadiri inavyokua kubwa na ku disturb biashara ya streaming

Kituo kinachofuata ni NKIRI
 
Ukiona muvie unaangalia bure online tofauti na youtube ujue ipo kiharamu
Mkuu kwa mtu aliyezoea kudownload movies free site za pirates hawezi kukuelewa

Sidhani kama siku hizi kuna biashara ya kudownload legally movies zaidi ya streaming
 
Mkuu hizo Site ulizozitaja hazina tofauti yoyote na FZmovies....... ni swala la muda tu

Site za wizi wa movies zipo nyingi lakini zinashughulikiwa kwa kadiri inavyokua kubwa na ku disturb biashara ya streaming

Kituo kinachofuata ni NKIRI
ndio maana nilikwambia hao wamiliki wake walikamatwa na wakatoka sasahivi hawasumbuliwi tena isipo kuwa wewe isp wako ndio atakusumbuwa maana ana amini kupakua movie ni haramu
 
Nilikuwa Vietnam mwezi July kwa kazi maalumu , Hanoi Na Hochmin,

Nchi ile ni maskini japo kunaanza kuwa na maendeleo kutokana na mchanganyiko wa wageni wa kizungu
 
ndio maana nilikwambia hao wamiliki wake walikamatwa na wakatoka sasahivi hawasumbuliwi tena isipo kuwa wewe isp wako ndio atakusumbuwa maana ana amini kupakua movie ni haramu
Mkuu naona HATUELEWANI
 
Kuna jamaa alikuwa anarusha matangazo ya mpira kutoka azam tv kwenye app yake walimdaka akapigwa faini milion 20🤣 uzuri wa online ukiwa smart kukudaka ningumu lakini wakikuvalia njuga kama unarusha maudhui ya watu inaweza kukuletea shida. Hata maudhui ya ngono yana copyright
 
Back
Top Bottom