Vifaa vya kijasusi vya aliyekuwa Jasusi Eli Cohen vyapatikana huko Syria!!!

Pre emptive strike haikutokana na taarifa za cohen bali wake wa viongozi wa juu misri waliokua waisrael wakihofia ndugu zao israel kufa,cohen kafa 1965,vita 1967, taarifa za Cohen ni syria, preemptive strike ilipigwa Syria..vinaendana vipi?
 
Jewish Arab au Arab Jewish linatumika vibaya, hili neno ni tusi kubwa sana ukimuuita Mmoja wao hilo jina anaweza kukuua
 
Yaani Story ya mwamba ni very interesting sana na mbinu Israel walitumia taifa lolote linaweza kutumia, yaani hii inatukumbusha kuwachunguza viongozi wetu
 
Pre emptive strike haikutokana na taarifa za cohen bali wake wa viongozi wa juu misri waliokua waisrael wakihofia ndugu zao israel kufa,cohen kafa 1965,vita 1967, taarifa za Cohen ni syria, preemptive strike ilipigwa Syria..vinaendana vipi?
Watu wengine mnajifanya wajuaji kwenye vitu ambavyo hata uelewa wake ni Zero kabisa!

Eli Cohen alikuwa mhimu sana kwenye historia ya Israel kwa sababu alikuwa mpelelezi wa Mossad aliyefanikiwa kupenya ngazi za juu za serikali ya Syria katika miaka ya 1960. Aliishi kwa jina la uwongo ( Nickname )Kamel Amin Thaabet na aliweza kujenga uhusiano wa karibu na maafisa wa juu wa kijeshi na kisiasa wa Syria. Kupitia uhusiano huu, alipata (Top secret)taarifa za siri za kijeshi za kimkakati ambazo zilikuwa za thamani kubwa kwa Israel.

Taarifa alizozipata ziliwasaidia Israel kujiandaa vyema kwa Vita vya Siku Sita mwaka 1967 Kwa mfano, alifichua maelezo kuhusu harakati za kijeshi za Syria kwenye Milima ya Golan ambazo zilikuwa kigezo muhimu cha ushindi wa Israel katika vita hivyo. Ushujaa wake na kujitolea kwake kulifanya awe mmoja wa wapelelezi nguli wa Israel, licha ya kwamba alikamatwa na kunyongwa na Syria mwaka 1965. Hivyo, mchango wake ulikuwa wa pekee katika kuimarisha usalama wa taifa la Israel.
 
Kivipi nfanyabiashara apate siri za jeshi?..mo dewji ana siri za jeshi?..
 
Kivipi nfanyabiashara apate siri za jeshi?..mo dewji ana siri za jeshi?..
Tatizo mmezoea upotoshaji ukweli ni huo nimeandika hapo juu!! Eli Cohen pamoja na yeye kunyongwa 1965 taarifa zake ndizo ziliwasaidia Israel kwenye Pre-emptive strike 1967 na ndio zilizowapa ushindi kwenye vita hivyo. Kipigo walichopata Syria kilidhoofisha sana majeshi ya waarabu wote!!
 
Preemptive strike ya israel 1967 ilipiga misri, cohen alikua misri na Jordan?!
 
Preemptive strike ya israel 1967 ilipiga misri, cohen alikua misri na Jordan?!
Narudia tena ni kweli Eli Cohen alikuwa Syria lakini Israel ilianza kushambulia Misri mnamo Juni 5, 1967, wakati wa Vita vya Siku Sita, ikianza na operesheni ya anga dhidi ya kambi ya jeshi la anga la Misri. Hii ilifuatiwa na mashambulizi dhidi ya Jordan, Syria, na baadaye Iraq, ambayo ilikuwa imeshiriki kwa kiwango kidogo

Mafanikio hayo yote yanatokana na taarifa za Eli Cohen alizozitoa kabla hajakamatwa pamoja na kwamba alinyongwa lakini Israel ilizitumia taarifa zake hivyo kuwapatia ushindi huo 1967.

Kama na hapa hutaelewa na kubeza juhudi za Eli Cohen basi mimi sina cha ziada kukufahamisha,
 
Iraq haikuwepo bana, misri kasarenda tarehe 8, Jordan 9, syria 10..tena syria hata hakushambuliwa,alivyoona misri kasarenda akaacha
 
Mwamba ni PM unajua Mengi AMBAYO nayapenda aisee
 
Video ikionyesha Eli Cohen akinyongwa huko Damascus Syria


View: https://x.com/eliafriatisr/status/1924577393613721729?s=61
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…