Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
JIMBO LA GANDO KUNUFAIKA NA VIFAA VYA MAJI SAFI NA SALAMA
Mbunge wa Jimbo la Gando Mhe. Salim Mussa Omar amesema kwamba amemtuma Katibu wa Ofisi ya Mbunge Jimbo la Gando Ndugu Mshani Ali Kachinga kukabidhi vifaa mbalimbali vya Maji katika Shehia tano vyenye thamani ya Shilingi Milioni 4,800,000.
Ndugu Mshani Ali Kachinga akishirikiana na viongozi wa CCM amekabidhi kwa wananchi vifaa, Matenki ya kuhifadhi Maji, Mashine za kupandisha Maji na Mipira Roli 7 katika Shehia Tano za Gando, Junguni, Kizimbani, Kinyasini na Magogoni.
Vifaa hivyo mbalimbali vya Maji Safi na Salama vina thamani ya Shilingi Milioni 4,800,000 ambavyo vimekabidhiwa mnamo tarehe 21 Mei, 2023 Viwanja vya Ukumbi wa Dolphin Bopwe, Wete, Pemba.
#GandoMpya