Watu 3 wamefariki na wengine 2 wako katika hali mbaya baada ya kile kinachosadikiwa ni kunywa pombe haramu huko Kimende, eneo-bunge la Lari, Kaunti ya Kiambu.
Kufuatia vifo hivyo, wakazi wa Kimende walifanya maandamano wakitaka hatua kali zichukuliwe dhidi ya uzalishaji na uuzaji wa pombe haramu, maandamano yaliyopelekea hata maafisa wa polisi kurusha mabomu ya machozi kutawanya wananchi.
Aidha wananchi wameibua maswali kuhusu jukumu la mamlaka za udhibiti, ikiwemo KEBS na KRA, katika kuhakikisha bidhaa za pombe zinazouzwa kwa umma zinakidhi viwango vinavyohitajika.
Takwimu zinaonyesha kuwa tatizo hili si la Kimende pekee. Ripoti zilizotolewa mwaka 2025 ziliripoti kuwa pombe haramu inakadiriwa kuchangia takriban 60% ya pombe inayotumiwa nchini Kenya, ongezeko la asilimia 27 kutoka makadirio ya mwaka 2022.
Mwaka 2026, data iliyowasilishwa kwa Bunge ilionyesha kuwa katika kipindi cha Januari 2024 hadi Mei 2026, zaidi ya 493,000 litres za pombe haramu zilikamatwa Rift Valley, huku Nyanza ikirekodi zaidi ya 160,000 litres na Western Kenya zaidi ya 134,000 litres.
Lakini maswali muhimu kila mmoja wetu anapaswa kujiuliza ni:
Je, mfumo wa sasa wa kudhibiti pombe haramu nchini unafanya kazi ipasavyo?
Je, mamlaka zinafanya vya kutosha kuzuia pombe haramu kabla haijawafikia watumiaji?
Je, operesheni dhidi ya wazalishaji na wasambazaji wa pombe haramu zinapaswa kuwa za mara kwa mara badala ya kuanzishwa baada ya vifo kutokea?
Na je, ni nani anapaswa kuwajibika pale bidhaa inayodaiwa kuwa haramu inapoingia sokoni na kusababisha madhara kwa wananchi?