Vifo Katesh; Je, Tanzania kuna milima mingine kama mlima Hanang?. Serikali imechukua hadhari gani?

Elimu yetu tunayoipata haitoshi kabisa kutufikisha Kanan. Watu wote wanatuongoza kwa kutumia elimu zao za kuzaliwa, hisia, na utashi wao binafsi au wa kundi lao. Wasomi wetu hawatofaitiani sana na wasiosoma kwenye kufikiri na kutenda. Ni waoga wa kila kitu isipokuwa kuiba muda na mali za mwajili wao. Hawawezi kudai haki zao Wala za wengine isipokuwa kuwa wanaharakati kwaajili ya kuongeza kipato chao. Professor aliyefunzwa vibaya atafundisha vibaya pia; mitaala mipya ni nani ataifundisha? vuluvulu tu.
 
Maeneo haya :- mwanza milimani nyumba na mawe inweza isiwe mvua likaja tetemeko,maeneo ya kitonga na nyang'oro,ni shida
 
Nyie endeleeni kusingizia volcano.
Huyo ni dragon.amejimbia hapo miaka zaidi ya milioni
Sasa.ameamua kuondoka kwa staili hiyo.kawaachia tope tu.
 
Maeneo haya :- mwanza milimani nyumba na mawe inweza isiwe mvua likaja tetemeko,maeneo ya kitonga na nyang'oro,ni shida
Majanga ni dili kwa wataalam wetu na wanasiasa. Hawataki kuzuia bali kutibu. Shida ingine Iko kwa wanasiasa wetu wa upinzani, hawana hoja za maana kwa taifa, ni opportunistics TU wanaovizia watawala wafanye jambo linalowachukiza wananchi ili wadandie humohumo. Kama serikali ikiamua kuwaondoa wananchi kwenye maeneo hatarishi kama vile milimani, mabondeni, kwenye hifadhi za wanyama au bodaboda na machinga, wapinzani ndio umewapatia hoja, wanageuka watetezi wao eti kusaka kura.
 
LOoooh!

Umetapika nyongo!
Kwa sasa nina maluweluwe mengi kichwani, ngoja nikuweke kiporo kwa sasa.
Ninahitaji akili tulivu ku'process' haya uliyoandika hapa, ambayo ninakubaliana nayo kiujumla wake.

Nina mifano mingi sana ya wasomi na maprofesa tuliowahi kuwa nao hapa kwetu. Wengi wa hawa watu walikuwa na elimu nzuri kabisa, ambayo hata ungewaweka katika taifa lolote duniani wangemudu vizuri tu kutokana na elimu yao hiyo.
Lakini hilo halikufua dafu katika mazingira ya kiTanzania. Ni lazima kutakuwepo na utofauti maalum kwa mazingira yetu yanayogeuza elimu nzuri kuwa takataka.

Kwa mfano: Jana ulimwona Kabugi Kalamaganda akivimbavimba na uzalendo wa kipekee kabisa chini ya uongozi wa kichaa mmoja hivi; kesho yake msomi huyo huyo anageuka na kuwa kama hakuwahi kuwepo kabisa chini ya mfumo wa kiongozi mwingine, tena asiye juwa hili wala lile kielimu. Usomi wa aina hii unashangaza sana.

Huu ni mjadala maalum unaotakiwa kujitegemea, kwa maoni yangu.
 
Professor anapewa wizara ya ujenzi, Leo anajenga barabara ya billion 70, baada miaka 2 kupita anaivunja hiyo barabara ikiwa mpya ili ajenge barabara ya mwendo kasi. Maana yake 70bil zimepotea tunatumia 160bil nyingine kwenye kipande kilekile ndani ya miaka 3. Baada ya mwaka mmoja anaivunja tena ili apitishe bomba la maji na mkongo wa taifa sehemu ya barabara. Huu ni wizi wa aina yake unaolidumaza taifa. Mipango mibovu. Saa nyingine pesa zote za kujenga, kuvunja na kujenga tena ni mkopo wenye riba.
 
Pia kwa kasi yetu ya kuzaana, wakati nchi haiongezeki, huko mbele watu watazidi kubanana tu.

Hivyo tunahitaji kupangilia vizuri sana both land use na family planning.

Enzi za kuzaana zaana ovyo tu na kuishi kwa kujua nchi kubwa tu hii zinaisha.
Wewe msomi heb tuambie hii dunia watu walianza kuishi lin? Acha watu wazaane hili dude haliwezi kujaa!
 

Hatuombei lakini hali kama hii iko kule mwanza siku pakiporomoka kule kilio chake kitakuwa si ch kitoto
 
Wewe msomi heb tuambie hii dunia watu walianza kuishi lin? Acha watu wazaane hili dude haliwezi kujaa!
This is simply mathematically unsound and too emotional to entertain.
 
Kiranga darasa tosha

Ova
 
Hatuombei lakini hali kama hii iko kule mwanza siku pakiporomoka kule kilio chake kitakuwa si ch kitoto
Ni kweli kuwa serikali itamjengea makazi mapya ya kudumu kwa kila mtu anaepatwa na janga? Tunaomba kabla ya kuwajengea wale wa katesh waanze na sisi wa bukoba tuliotangulia kukumbwa na tetemeko mwaka juzi.
 
Wewe msomi heb tuambie hii dunia watu walianza kuishi lin? Acha watu wazaane hili dude haliwezi kujaa!
Dunia ilivyotengenezwa ilitakiwa isijae, lakini binadamu kashaharibu ecolojia. Ilitakiwa kuwe na uwiano kati ya wanaosaliwa na wanaokufa, wanaohama na wanaohamia lakini Sasa haiwezekani tena tumeshaharibu the natural history ya mambo mengi. Dunia itajaa na kupwa. Idadi kubwa ya watu ni nzuri kwa uchumi TU lakini ni mbaya sana kwa mazingira na huduma za kijamii. Kiuchumi ni nzuri kwakuwa kila mtu anakula chumvi hivyo mwenye chumvi atatajirika kwakuwa chumvi yake inaliwa na watu wengi.

Dunia itajaa haraka kama kila kaburi litakuwa la zege na marumaru na mtu mmoja TU kujenga nyumba za zenge nyingi bila sababu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…