Vifo Katesh; Je, Tanzania kuna milima mingine kama mlima Hanang?. Serikali imechukua hadhari gani?

Vifo Katesh; Je, Tanzania kuna milima mingine kama mlima Hanang?. Serikali imechukua hadhari gani?

Ukishaishi kwa kuamini kudra za Mwenyezi Mungu utajenga popote pale.

After all, unaweza kuacha kujenga milimani ukajenga sehemu tambarare, lakini kwa kudra tu ukapigwa radi vilevile.

Hii mentality ya kuishi kwa kudra ndiyo inatugharimu.
kwahiyo tuishi kwa kudra?
 
Tamaa za fedha na ujinga wa kutoiona kesho vinasababisha maafa siku za usoni
Hata maeneo yaliyoachwa wazi ili kuhifadhi watu wakati wa majanga yote sasa hivi ni mali ya chama, ni maegesho ya magari au ni baa au yameuzwa.
 
Kule kwetu tulizaliwa wengi, watoto 20 kwa wanawake 3 wa baba, lakini wote tulikwenda shule kwakuwa watoto wote tulikuwa na kazi za kufanya kule shambani, kwenye mifugo, kwenye mizinga ya baba na dukani. Tulikuwa tunalima sana, kuchunga sana, kukamua sana, kulisha kuku sana, kulinda tumbili sana, kurina asali sana na kulisha kuku sana kiasi kwamba hatukuwa na shida ya chakula wala ada ya shule na chuo. Bro, ni sera tu mbovu.
Sasa, wingi au uchache wa watu hauwezi kujadiliwa nje ya muktadha wa sera za uchumi, teknolojia na mipango ya nchi.

Kwa sera za uchumi, teknolojia na mipango ya Tanzania leo, hatuhitaji watu wengi zaidi.

Tunahitaji kuwa na mipango mizuri ya kuweza kuwatumia hawa watu tulionao kwanza kabla ya kuongeza watu wengi zaidi.

Ukiongeza watu kwa kasi kubwa bila ya kupanga jinsi ya kuwatumia, utakuwa unatengeneza time bomb tu.

Hapo ndipo namaanisha kwamba tunazaana sana kuliko uwezo wetu wa kuitumia nguvukazi ya watu wanaozaliwa na kuipangia kuishi maisha mazuri.

Huo mfano wa kwenu mliweza kuishi vizuri kwa standards za agrarian society, watanzania wengi walikuwa masikini lakini hawakujijua kwa sababu waliishi almost kwa subsistence farming na agrarian societies, vijijini.

Leo tunaenda dunia ya teknolojia, usomi, uchumi wa kimataifa etc, watu kuzaa watoto 20 bila ya mpango wa kwenda na dunia ya leo ni kutengeneza mzigo mkubwa wa umasikini.
 
Tz kuja kufikia kubanana hy bado sana, hata tukiwa 150M bado ardhi ipo kubwa sana tuu labla useme kubanana kwenye majiji na sio Tz nzima
Overpopulation si kubanana ardhi tu.

Mfano.

Nchi A yenye ardhi kubwa, lakini elimu duni, teknolojia ndogo, inayotegemea kilimo cha mvua za msimu kisichotumia teknolojia kubwa na kukata miti sana ili kupata kuni, inaweza kuwa overpopulated na idadi ile ile ya watu ambayo kwenye nchi B ndogo zaidi, ambayo ina elimu bora, inatumia kilimo cha teknolojia kubwa na umwagiliaji, na nishati ya nuclear, na haina shida ya kukata miti ili kupata kuni inakuwa underpopulated.

Kwa hiyo, overpopulation ni dhana kubwa zaidi ya kuangalia idadi ya watu na ukubwa wa nchi tu.
 
majanga haya ni mitaji
Inabidi kukubaliana nawe; maana tumeona jinsi mkasa huu ulivyotumika na wahusika kuutumia kuwa mtaji.

Lakini kinacho sikitisha ni kwa hao waliopatwa na mkasa kutotambua kwamba wanatumika kama mtaji.
 
OLDONYO LENGAI ni hatari zaidi kwasababu ni hai na kuna wakati huwa inatoa moshi mweusii
 
OLDONYO LENGAI ni hatari zaidi kwasababu ni hai na kuna wakati huwa inatoa moshi mweusii
Usichanganye volcano na landslide (Maporomoko ya ardhi). Mlima Hanang umekumbwa na landslide na Oldonyo Lengai ni volcano!
 
Nitakuwa kinyume na wewe.Mimi naona nchi zenye idadi kubwa ya watu ndiyo zenye maendeleo (kiuchumi) makubwa hapa duniani.
Halafu kuna jibu hapa:
Maendeleo hayaji kwa idadi kubwa ya watu, maendeleo yanakuja kutokana na kujua kutumia watu na kupanga uchumi vizuri kulingana na idadi ya watu.

Sasa sijui kama kuna elimu ya kutosha iliyobadishwana hapa kufikia mwafaka.

Mmoja ni "BabuMkubwa", ambaye nachukulia kuwa ni mtu wa makamo ya kutosha na kuwa na upeo stahiki kutokana na uzoefu wa maisha, na uzoefu wa kimazingira kumwezesha kuwa na ufahamu wa uhusiano kati ya wingi wa watu na uwepo wa maendeleo miongoni mwa watu hao.

Sitamzungumzia wa pili, kwa sababu anajulikana vizuri miongoni mwa washiriki katika jukwaa hili.

Nimevutiwa na mabadilishano ya mawazo kati ya hawa wawili, kwa sababu moja tu; kwamba pamoja na kuwa nchi huru miaka zaidi ya 60, na kuwa na mamlaka yetu wenyewe juu ya elimu ya watu wetu; bado inaonekana kuwepo upungufu mkubwa sana katika jamii yetu, kuweza kutambua maswala ambayo ni rahisi kabisa kuhusu hali yetu duni kimaendeleo.
Kuna nyakati tunajifikiria tumepiga hatua mbele zaidi kimaendeleo kuliko wakati mwingie wowote tokea uhuru. Lakini unapokutana na maswala ya aina hii, na kujua kuwa ndani ya jamii bado kuna upungufu mkubwa wa uelewa juu ya maswala ya msingi kabisa kama hili; halafu unakumbana tena na wengine wakijitangaza kuwa "chawa" juu ya viongozi wetu wanaoshindwa kutufumbua macho kielimu, inabidi kujiuliza maswali mengi kama kweli safari yetu ya maendeleo inakwenda mbele au inarudi kinyumenyume.

Ni mawazo tu, yaliyo niijia akilini baada ya kusoma mabadilishano kati ya hawa wawili.
 
Hata maeneo yaliyoachwa wazi ili kuhifadhi watu wakati wa majanga yote sasa hivi ni mali ya chama, ni maegesho ya magari au ni baa au yameuzwa.
Very true.

Tubadilike au tubadilishwe
 
Sasa milima kama ya Hanang iko mingapi ili walioko kwenye milima hiyo wasisubiri kujifunza kwa makosa yao wenyewe? watumie darasa hili hili la katesh.
Ni huo pekee . Hakuna mwingine.
 
Kuna visiwa vya kwenye bahari ya Pacific vinaelekea kuzama chini ya bahari kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa na usawa wa bahari kupanda.

Kwa hiyo, vinapanga kuendelea kama nchi mtandaoni tu baada ya kuzama baharini.

Usije kushangaa visiwa hivi vikapata maendeleo kama nchi za mtandaoni, bila ya kuwa na radhi, wakati sisi tuna ardhi lakini hatuna maendeleo.
Status ya visiwa vya bahari ya Hindi ikoje, hasa visiwa vyetu pendwa
 
Asante kwa video mkuu.

Inasikitisha sana.

Pole nyingi kwa wote waliopatwa na janga hili.
Kusombwa kwa nyumba nyingi ni ushahidi mwingine wa uholela kwenye sekta ya ujenzi na makazi nchini. Hazikuwa nyumba bali matope TU (matembe). Ndio maana watu wanashangaa kuona nyumba za ibada kanisa na msikiti zimebakizwa bila kusombwa. Ukweli sio miujiza kubaki bali zilikuwa imara, zimejengwa vizuri kuliko nyumba zilizozolewa. Uholela huu kwenye wizara ya ujenzi unasababisha vifo vingi sana na hasara kwa wananchi na serikali pia. Waziri wa ujenzi ajiuzulu.
 
Inabidi kukubaliana nawe; maana tumeona jinsi mkasa huu ulivyotumika na wahusika kuutumia kuwa mtaji.

Lakini kinacho sikitisha ni kwa hao waliopatwa na mkasa kutotambua kwamba wanatumika kama mtaji.
Nyumba zao zilikuwa duni sana ndio maana zilisombwa kirahisi, ni matope yaliyokutana na matope mengine kutoka mlimani. Sekta ya ujenzi Ina matatizo pia, watu wanajijengea nyumba kiholela kujenga msingi, kutana na mapaa hafifu mno.
 
Halafu kuna jibu hapa:

Sasa sijui kama kuna elimu ya kutosha iliyobadishwana hapa kufikia mwafaka.

Mmoja ni "BabuMkubwa", ambaye nachukulia kuwa ni mtu wa makamo ya kutosha na kuwa na upeo stahiki kutokana na uzoefu wa maisha, na uzoefu wa kimazingira kumwezesha kuwa na ufahamu wa uhusiano kati ya wingi wa watu na uwepo wa maendeleo miongoni mwa watu hao.

Sitamzungumzia wa pili, kwa sababu anajulikana vizuri miongoni mwa washiriki katika jukwaa hili.

Nimevutiwa na mabadilishano ya mawazo kati ya hawa wawili, kwa sababu moja tu; kwamba pamoja na kuwa nchi huru miaka zaidi ya 60, na kuwa na mamlaka yetu wenyewe juu ya elimu ya watu wetu; bado inaonekana kuwepo upungufu mkubwa sana katika jamii yetu, kuweza kutambua maswala ambayo ni rahisi kabisa kuhusu hali yetu duni kimaendeleo.
Kuna nyakati tunajifikiria tumepiga hatua mbele zaidi kimaendeleo kuliko wakati mwingie wowote tokea uhuru. Lakini unapokutana na maswala ya aina hii, na kujua kuwa ndani ya jamii bado kuna upungufu mkubwa wa uelewa juu ya maswala ya msingi kabisa kama hili; halafu unakumbana tena na wengine wakijitangaza kuwa "chawa" juu ya viongozi wetu wanaoshindwa kutufumbua macho kielimu, inabidi kujiuliza maswali mengi kama kweli safari yetu ya maendeleo inakwenda mbele au inarudi kinyumenyume.

Ni mawazo tu, yaliyo niijia akilini baada ya kusoma mabadilishano kati ya hawa wawili.
Mwenye akili timamu ni yule anaejiuliza mwenyewe maswali kuhusu "ni kwanini tuko hivi na kwa nini tumebaki hivi tulivyo kiuchumi, kielimu, kiafya, kiuzazi,.......?". Ataendelea kujiuliza mwenyewe "Ni kwanini Afrika yote inafanana fanana kimaendeleo na mambo Yao mengine yote?" Ataendelea kujiuliza "ni kwanini hata nchi zilizobadilisha vyama vyao tawala kama vile Zambia, Malawi, Kenya, Liberia, DR Congo, Uganda, nk hata wao bado hali Yao kiuchumi Iko vilevile TU?"

Ukishapata majibu ya maswali hayo ndiyo uje na majibu ya mjadala kati ya uhusiano kati ya idadi ya watu na maendeleo.
 
Usishonw koti 1 nchi nzima. Kila mahali pana upekee wake. Jinsi mlima Hanang ulivyoanza ni tofauti na meru nk. Jielimishe.

Sehemu ya Mji wa katesh upo kwenye mkondo wa maji haswa wale watu kwa kwanza. Ulipopanuka umeelekea srhemu za miinuko na mabonde. Miji mingi ipo hivyo.
 
Mwenye akili timamu ni yule anaejiuliza mwenyewe maswali kuhusu "ni kwanini tuko hivi na kwa nini tumebaki hivi tulivyo kiuchumi, kielimu, kiafya, kiuzazi,.......?". Ataendelea kujiuliza mwenyewe "Ni kwanini Afrika yote inafanana fanana kimaendeleo na mambo Yao mengine yote?" Ataendelea kujiuliza "ni kwanini hata nchi zilizobadilisha vyama vyao tawala kama vile Zambia, Malawi, Kenya, Liberia, DR Congo, Uganda, nk hata wao bado hali Yao kiuchumi Iko vilevile TU?"

Ukishapata majibu ya maswali hayo ndiyo uje na majibu ya mjadala kati ya uhusiano kati ya idadi ya watu na maendeleo.
Mkuu,

Kama hujui jinsi ya kutumia nguvukazi yako ya sasa, kuongeza watu ambao wataongeza utegemezi bila kuwa productive ni kuongeza tatizo.

Tunaweza kujua 10 si square root ya 2, hata kabla hatujajua square root ya 2 ni nini.

Tunaweza kujua jibu fulani si jibu sahihi hata kabla hatujajua jibu sahihi ni lipi.

Tunaweza kujua kwamba, jibu la kutaka kumaliza umasikini kwa kuongeza watu, bila ya kuwa na mipango sahihi ya kutumia nguvukazi zao, si jibu sahihi, hata kabla hatujajua jibu sahihi ni lipi.
 
Maendeleo hayaji kwa idadi kubwa ya watu, maendeleo yanakuja kutokana na kujua kutumia watu na kupanga uchumi vizuri kulingana na idadi ya watu.

Unaweza kuwa na watu wengi, lakini hujajipanga, unaongeza njaa tu.

Ingekuwa maendeleo yanatokana na wingi wa watu, India ingekuwa imeendelea kuliko Marekani na Nigeria ingekuwa imeendelea kuliko Italy.

Upo sahihi sana, kuwa na population inategemea watu hao wanauwezo gani kujikwamua kiuchumi ili kusaidia uchumi wa nchi kuinuka! Kwa mfano hata population kubwa iliyopo serikali ingewekeza kwenye uzalishaji wa malighafi nyingi zinazoagizwa nje, zikazalishwa Tanzania zikawa processed hapa hapa kwa sababu ya population kuwa zikatumika hapa hapa, na zinazozidi tuka export nje ya nchi kwa wingi uchumi wa nchi ungekuwa sana.

Wataalamu waangalie namna ya kupata malighafi, viwanda vijengwe kwa ajili ya processing,, tutumie vitu vyetu tunavyozalisha wenyewe tu, na tu export kwa wingi kama uchumi wetu haujakuwa maradufu.
 
Back
Top Bottom