Mwenye akili timamu ni yule anaejiuliza mwenyewe maswali kuhusu "ni kwanini tuko hivi na kwa nini tumebaki hivi tulivyo kiuchumi, kielimu, kiafya, kiuzazi,.......?". Ataendelea kujiuliza mwenyewe "Ni kwanini Afrika yote inafanana fanana kimaendeleo na mambo Yao mengine yote?" Ataendelea kujiuliza "ni kwanini hata nchi zilizobadilisha vyama vyao tawala kama vile Zambia, Malawi, Kenya, Liberia, DR Congo, Uganda, nk hata wao bado hali Yao kiuchumi Iko vilevile TU?"
Ukishapata majibu ya maswali hayo ndiyo uje na majibu ya mjadala kati ya uhusiano kati ya idadi ya watu na maendeleo.
Mkuu 'kavulata', mchango wako huu unazidi kuninyima utulivu wa mawazo. Nimekwisha andika juu yake na kuondoka; lakini bado akili imebaki tu kwenye haya uliyo andika hapa.
Mimi najibu kifupi tu kwa haraka. Tatizo ni UONGOZI.
Uongozi usiokuwa na maono, uliochanganyika na kujinufaisha wenyewe badala ya kunufaisha nchi zao.
Pili, kamwe hatuwezi kutotaja mazingira yanayotuzunguka. Kama mazao yetu na vyanzo vyetu vya mapato hatuna uwezo wa kuhakikisha vinaendelea kuzalisha ili tupate mitaji ya kujiendeleza, tutaanzia wapi. Kama uchumi wa dunia umeporomoka, wa kwetu unaporomoka zaidi.
Hapa Tanzania tulikuwa mashuhuri enzi zile katika uzalishaji wa mkonge na pamba. Mjapan kagundua nyuzi za 'nilon', soko letu likadoda. Brazil alipokuwa kinara wa uzalishaji wa kahawa, kahawa yetu ikadoda; n.k., .
Taifa linategemea utalii kama chanzo mashuhuri cha pato. Anapoingia COVID - 19; hapo utalaumu vipi kuvurugika kwa shughuli za pato la nchi hizi?
Sasa kosa lipo wapi? Linarudi palepale kwenye uongozi mbovu usiokuwa na maono; maono ya kujipanga vizuri ili kuhimili majanga haya yanapo tokea. Elimu yetu inakuwa mbovu, haitoi mazao yanayolenga kupambana, badala yake tunazalisha mazao yanayo jitambulisha kuwa "CHAWA" wa kunyonya uchafu toka kwa hao viongozi wabovu.
Tatu, ni vizuri pia kuvuta subira. Tazama nchi zingine duniani zilipitia wapi. Portugal ya miaka ya 60; 80; pamoja na kuwa na makoloni mbalimbali nje, lakini ilikuwa ni nchi maskini tu! Hivyo hivyo na Hispania na kwingineko. Nchi jirani zilipoanza kuinuka, na wao zikawainua.
Nchi za Asia, kulikuwa na Japan pekee akitamba maeneo hayo wakati Korea Kusini na wengineo wakiwa katika hali duni kabisa hadi kwenye miaka ya 60 hivi. China walikuwa wakihangaika tu, Vietnam vilevile; Thailand, Indonesia na kwingineko. Mazingira ya leo ni tofauti kwa nchi hizo.
Kwa hiyo, hata sisi tunakwenda hivyo hivyo, hasa kwenye nchi zitakazo bahatika kuwa na viongozi wenye uchungu na hali za maisha ya wanachi wao na kuweka sera zinazohakikisha mafanikio yanapatikana haraka.
Isingekuwa CCM wanavyoturudisha nyuma zaidi, Tanzania ingekuwa ni miongoni mwa nchi za kwanza kabisa katika Afrika kuondokana na uduni wa maisha ya wananchi wake; kwa sababu kila nyenzo muhimu za kutuwezesha kufanya hivyo tunazo; tunacho kikosa ni uongozi imara wa kutupeleka huko haraka.
Wingi wa watu siyo hoja muhimu, ingawaje sioni sababu kwa Tanzania sasa hivi kubana ongezeko la watu.