Vifo Katesh; Je, Tanzania kuna milima mingine kama mlima Hanang?. Serikali imechukua hadhari gani?

Vifo Katesh; Je, Tanzania kuna milima mingine kama mlima Hanang?. Serikali imechukua hadhari gani?

3. Je, kuna mifumo gani ya kutaarifiana kama ving'ora kama likitokea janga?

Kinga ni bora kuliko kiba hii tunayoiona.
Mifumo haipo japo ilitakiwa kuwepo chini ya ofisi ya Waziri Mkuu.
Ukisoma Sendai Framework for Disaster Risks Reduction (SF-FDRR) utaona miongozo ya nini kifanyike kabla, wakati wa na baada ya majanga/maafa!
Yote tunayofanya Tanzania hayamo ndani ya Sendai Framework for Disaster Risks Reduction 2015-2030!
 
Tunasubiri vifo ili turushe helkopta kuangalia kiwango cha uharibifu na idadi ya waliokufa badala ya kunusa mapema hatari na dalili vifo.

Kwa kilichotokea Hanang ni matokeo ya mipango mibaya ya watanzania wenzetu tunaowalipa kwa kazi ya kutulinda na majanga. Kuna idadi kubwa ya watanzania ambao wameruhusiwa kujenga chini na juu ya milima, mabondeni, kwenye njia za maji na wanyama. Watu hawa wamepewa vibali vyote ama vya kujenga, au kuingiza umeme na maji kwenye nyumba zao bila kupewa onyo la aina yoyote wala elimu ya namna ya kuishi kwenye maeneo hayo.

Maswali:,
1. Je, baada ya maafa ya Katesh, watu waendelee kujenga na kuishi kwenye maeneo yao yaleyale yaliyokubwa na janga au wahamie kwingine?
2. Je, Tanzania hakuna watanzania wanaoishi kwenye maeneo yanayofanana na maeneo ya Katesh?
3. Je, kuna mifumo gani ya kutaarifiana kama ving'ora kama likitokea janga?

Kinga ni bora kuliko kiba hii tunayoiona.

Mingine wataigundua yakishatokea
 
Tuanzie na mlima maarufu barani afrika uliopo tanzania, watu wamejenga vijiji kwenye slope zake kunaitwa uchagani. Kuna upareni mwendo ni uleule kujenga kwenye miteremko ya milima, milima ni mingi na watu wamejenga chini yake. Kuna milima inamwaga maji yake bwawa la nyumba ya mungu lakini kuna vijiji vimejengwa kwenye mapito ya maji hayo. Ole wao siku inyeshe mvua ya haja kubwa hayo maji yake itakuwa ni balaa yatasomba kijiji kizima. Kuna watu akili zao wanajua wenyewe ziliko, watajengaje makazi kwenye njia za mapito ya maji wakati kuna viashiria vyote kuonesha hapo ni hatari? Wengine wanajenga kwenye mikondo ya matetemeko ya ardhi, maporomoko ya udongo, kwenye upepo mkali, dhoruba, sehemu zenye mafuriko/ukame na hawana njia za kupambana na majanga hayo
 
images - 2023-12-06T145448.402.jpeg
 
Tatizo unaangalia eneo tu.

Hujaangalia arable land. Hujaangalia irrigation. Hujaangalia technology.

Unaweza kuwa na eneo kubwa, huna uwezo wa kulitumia vizuri, huna technology,ukawa na tatizo kwamba kwa level yako ya maendeleo, uko overpopulated.

Halafu akaja mtu ana population kama wewe eneo dogo, anajua kulitumia, ana technology kubwa, akawa underpopulated.

Japan wana watu zaidi ya milioni 125, karibu mara mbili ya population ya Tanzania.

Tanzania ina 365,756 sq mi Japan ina 145,937.06 sq mi, lakini Japan ina tatizo la kuongeza watu, Tanzania ina watu wengi sana wasio na kazi na haitakiwi kuongeza watu zaidi kwa kasi wakati hawa waliopo tu hatujui tufanye nini.

Katika dunia ambayo watu wanaweza kujenga miji kwenda juu kama Tokyo, suala la overpopulation si la ukubwa wa nchi tu, ni suala la teknolojia na uwezo wa kukabiliana na mazingira.

Kwa teknolojia yetu ambayo hata kilimo cha umwagiliaji kinatushinda, bado tunakata miti kupata kuni kamansource of energy, we are overpopulated.
Asante mkuu,
Nimeipenda sana analysis yako nakunukuu

"Tanzania ina 365,756 sq mi Japan ina 145,937.06 sq mi, lakini Japan ina tatizo la kuongeza watu, Tanzania ina watu wengi sana wasio na kazi na haitakiwi kuongeza watu zaidi kwa kasi wakati hawa waliopo tu hatujui tufanye nini"

Umeweka na data kabisa nimependa uchambuzi wako na umeelezea kindaki ndaki matatizo yetu ya tangu kupata uhuru 😊☺️

✌️✌️
 
Pia kwa kasi yetu ya kuzaana, wakati nchi haiongezeki, huko mbele watu watazidi kubanana tu.

Hivyo tunahitaji kupangilia vizuri sana both land use na family planning.

Enzi za kuzaana zaana ovyo tu na kuishi kwa kujua nchi kubwa tu hii zinaisha.
Mkuu umeongea vyema lkn nchi hii ina lack mipango ndio tatizo mama kwa kweli.
Kuna maeneo au mikoa ilitakiwa kusiwepo makazi kabisa maana kuna support kilimo almost mkoa mzima au wilaya nzima.
Yaani sisi kama nchi tuna Dhani maisha yatakuwa hivi milele wakati mabadiliko ni mengi sana.
Kizazi kijacho kitatumia ngivu nyingi sana kuweka mambo sawa.
 
Ukiongelea Hatarishi Mount Kilimanjaro is Dormant kuna siku itafanya yake.....
 
Nafikiri ile ilo poromoshwa na maji ni volcanic ashes..

Milima mingi TZ ipo kwenye miamba migumu... La, Mwanza kungekua hakuna mtu anaishi. Wote wako milimani...au Mbeya.
Sasa milima kama ya Hanang iko mingapi ili walioko kwenye milima hiyo wasisubiri kujifunza kwa makosa yao wenyewe? watumie darasa hili hili la katesh.
 
Nitakuwa kinyume na wewe.Mimi naona nchi zenye idadi kubwa ya watu ndiyo zenye maendeleo (kiuchumi) makubwa hapa duniani.
Kwa kuongezea..

Ili nchi iendelee inahitaji vitu vifuatavyo; WATU, ARDHI, SIASA SAFI, NA UONGOZI BORA. Kwa sasa Tanzania imebaki vitu viwili tu...
 
Maendeleo hayaji kwa idadi kubwa ya watu, maendeleo yanakuja kutokana na kujua kutumia watu na kupanga uchumi vizuri kulingana na idadi ya watu.

Unaweza kuwa na watu wengi, lakini hujajipanga, unaongeza njaa tu.

Ingekuwa maendeleo yanatokana na wingi wa watu, India ingekuwa imeendelea kuliko Marekani na Nigeria ingekuwa imeendelea kuliko Italy.
Kwa kuongezea,

Ili nchi iendelee inahitaji vitu vifuatavyo; WATU, ARDHI, SIASA SAFI, NA UONGOZI BORA. Kwa sasa Tanzania imebaki vitu viwili tu...
 
Mkuu umeongea vyema lkn nchi hii ina lack mipango ndio tatizo mama kwa kweli.
Kuna maeneo au mikoa ilitakiwa kusiwepo makazi kabisa maana kuna support kilimo almost mkoa mzima au wilaya nzima.
Yaani sisi kama nchi tuna Dhani maisha yatakuwa hivi milele wakati mabadiliko ni mengi sana.
Kizazi kijacho kitatumia ngivu nyingi sana kuweka mambo sawa.
Kwa kiasi kikubwa nchi hai lack mipango. Tuna mipango mingi tu.

Nchi ina lack utekelezaji wa mipango.

Miaka ya 1980s wakati tulishaanza kuhamisha makao makuu kwenda Dodoma, Wa Nigeria walikuja kupata idea kama yetu. Walitaka kuhamisha mji mkuu kutoka Lagos kwenda Abuja.

Wakaja kujifunza kwetu, wakachukua makabrasha kuyafanyia kazi.

Wakaenda kuhamisha mji mkuu wao kutoka Lagos kwenda Abuja. Wakamaliza.

Sisi tuliowapa mipango tukawa bado hatujamaliza zoezi kwa miaka mingi, mpaka leo mabalozi karibu wote bado wako Dar. Wanaona hatujawa serious kwenye hili.

Tumepanga mipango miingi, utekelezaji mdogo sana.

Kuna jamaa mmoja alikuwa mwanaharakati wa elimu, jamaa alikuwa well connected kitaa anakijua, halafu kasoma mpaka Harvard mambo ya kimataifa yuko vizuri. Basi alikuwa anafanya activism sana mambo ya elimu.

JK akamuona. Akasema wewe nakitaka uje juwa mshauri wangu mambo ya elimu. Jamaa akasema naam, hapa sasa nimepata sikio la rais, mambo yataenda vizuri, tutabadili mengi.

Basi jamaa kila akimshauri JK, JK anamwambia hilo? Hilo tunalijua tangu miaka 10 nyuma, mtafute Katibu Mkuu wizara ya elimu atakupa makabrasha yote. Jamaa akimshauri JK kitu kingine, anaambiwa, hilo? Hilo tulishafanya utafiti Mzumbe, mtafute Mkuu wa Chuo atakupa makabrasha yote.

Yani jamaa alifikiri yeye anajua mambo mengi, serikali haijui tu, na akipata nafasi ya kushauti serikali, watabadili mengi.

Akaja kugundua kuwa, mambo mengi aliyotaka kushauri, serikali ilikuwa inayajua, tena zaidi ya alivyoyajua yeye.

Tatizo halikuwa kujua, tatizo lilikuwa utekelezaji.

Jamaa alijiuliza, sasa hapa nafanya nini? Ikabidi aache ile kazi, kwa sababu hakuna alichokuwa anafanya.

Makabrasha kibao yanapata vumbi, studies kibao watu wanefanya na kushauri.

Tatizo ni kwenye utekelezaji huko.
 
Back
Top Bottom