T14 Armata
JF-Expert Member
- Mar 7, 2017
- 12,362
- 41,886
Huwa nabishana na watu msimamo wangu ni matatizo ya Congo hayatokani na wazungu. Wazungu wamekuja kutokana na mwaya ulioachwa wazi na tabia za hawa Waafrika wenzetu. Congo sijui ina laana gani kila kitu wanafanya vibaya.Wapumzike salama waliofariki ila najiuliza Congo kuna laana gani mbona kila janga wao!? Treni yao wanapanda na wanyama na wanakaa juu ya mabehewa, meli zao ni hivyohivyo pia! Kuna namna ile jamii inapaswa kuelimishwa istaarabike.
Nchi kila siku inalalamika kuteswa na Rwanda wakati ka-Rwanda kanazidiwa na mkoa wa Tabora.
Hivi nchi kubwa kama Congo inashindwa kulinda mpaka wa eneo dogo linalozidiwa na Tabora asitoke kitu au kuingia kitu bila uangalizi wao.