Vifo vya ghafla vya mamilionea vijana nchini Zimbabwe katika mtazamo wa kiroho

Vifo vya ghafla vya mamilionea vijana nchini Zimbabwe katika mtazamo wa kiroho

WICKNELL CHIVAYO HAKUFA NA WANAWE!

Taarifa zinazosambaa mitandaoni ya kuwa mfanyabiashara maarufu nchini Zimbabwe, Wicknell Chivayo aliuliwa pamoja na wanawe katika ya Helikopta kule Marondera, Zimbabwe sio sahihi.

Ukweli ni kuwa watu waliopoteza maisha katika ajali ile ni watano na wala sio sita. Watu hao ni Wicknell Munodaani Chavayo, Lucy Muteke (mke wa Chivayo), Saneliswe Magagula (mlinzi au msaidizi wa Chivayo), Calvin Soda (rubani) na Courage Mutavirwa (rubani mwenza). Hii ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Polisi nchini Zimbabwe muda mfupi uliopita.
 
1790929265671.jpg
 
JE, NANI KACHUKUA KICHWA CHA CHIVAYO?

Taarifa zinaarifu ya kuwa Wicknell Chivayo na mke wake Lucy Muteke ('Lulu') watazikwa bila ya vichwa vyao kwa sababu havikupatikana. Ila maelezo yanayotolewa na baadhi ya watu ni kuwa miili yao ilisaharibika sana na mingine ilikuwa inaendelea kuungua hata baada ya hiyo Helikopta kuanguka masaa kadhaa baadaye.

Lakini swali la kujiuliza hapa ni kuwa iweje pia vipande vingine vya miili yao ipatikane lakini vichwa vyao visipatikane? Lakini katika hali ya kawaida, mifupa pamoja na mafuvu ni viuongo ambavyo huchelewa sana kuharibika iwe kwa moto au kwa kuoza?

Jambo linaloweza kueleweka ni kama eneo la hajali hawakupata chochote isipokuwa majivu tu? Lakini hakuna taarifa iliyotolewa na uokozi kuwa walizoa majibu tu. Katika eneo la tukio kuna ushahidi wa picha zinazoonyesha mabaki ya viatu vya Chivayo pamoja na mabeki yake?

Je, iweje moto huo uunguze vichwa lakini viatu na vitu vingine viwepo? Je, vichwa vilikatwa huko huko angani na kupeperushwa kabla ya Ndege kuanguka? Lakini ni kwa nini taarifa ya muhimu kama hiyo isitolewe na Serikali badala yake inatolewa na familia?
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Itunge, Dar es Salaam; 5 Oktoba 2026; Saa 7:35 adhuhuri.
 
Kutoka kwa Edo Kumwembe

Huyu ni Ginimbi, alikuwa mfanyabiashara wa Zimbabwe mwenye utata na rafiki wa karibu wa Wicknell Chivayo.

Alifariki katika ajali ya barabarani siku ya Jumapili, Novemba 8, 2020. Jamaa alikuwa tajiri sana!, alikuwa akifanya sherehe za siku ya kuzaliwa mara kwa mara.

Leo anapoandaa sherehe kubwa sana; unapodhani sherehe imekwisha, huwapeleka watu wote nyumbani kwake kijijini ili kuendeleza sherehe hiyo kwa siku nyingine tatu mfululizo.

Wakati wa ajali hiyo mbaya, alikuwa akiendesha Rolls-Royce Wraith majira ya saa 11 alfajiri. Alikuwa amemaliza sherehe moja na alikuwa akielekea kwenye sherehe nyingine.

Alifariki papo hapo pamoja na marafiki zake watatu - Karim, Elisha na mpenzi wake Moana.
Baada ya kifo chake, inadaiwa baba yake alikuta kiasi kikubwa cha fedha chenye mabaki ya damu ndani ya nyumba yake.

Dada yake, Juliet, ambaye alirithi utajiri wake, naye alifariki katika ajali kama hiyo alipokuwa akisafiri kutoka Tanzania kwenda Zimbabwe.
Tangu wakati huo, inasemekana hakuna mwanafamilia aliyethubutu kugusa au kurithi mali zake.

Hata magari yake ya kifahari bado yapo katika jumba lake la kifahari huko Harare, bila kuguswa! Ginimbi alidaiwa kuwa mwanachama wa Illuminati.

Inasemekana hata alinunua jeneza la Versace lenye alama ya Illuminati iliyochorwa juu yake. Alikuwa amelihifadhi jeneza hilo katika jumba lake huko Harare.

Thamani ya utajiri wake ilikadiriwa kuwa dola milioni 500 za Marekani. Cha kushangaza ni kwamba jina lake halisi lilikuwa Genius Kadungure.

Nadharia nyingi ziliibuka kuhusu kifo chake, na huenda nadharia nyingi pia zikaibuka kuhusu kifo cha Sir Wicknell Chivayo.

Hata hivyo, kumbuka kwamba katika maisha, uchaguzi una matokeo. Daima chagua njia ya haki.
1791215541611.jpg
 
Back
Top Bottom