Vifo vya vijana hawa miaka 80 na early 90 huko ushuani, Oysterbay

Asante sana kwa mshairi mwema kwake huyu mdau.
 
Kabisa na watu wa hivi huwa wana maumivu moyoni na huja kutolea wengine ili waowaweze jisikia vizuri.
 
Wale wali hama pale , lakini miaka ya 90 nadhani wali haimia maeneo ya Mbezi Beach kama sikosei ,Huyo dogo wa soksi mpaka magotini , ni yupi kati ya wale wawili ?wewe ulisoma na Tom? .
Mchezo wa simu aisee duh, kwetu sijui bill ilikua inalipwa na serikali au dingi , maana dah, tulikua tuna piga story kwenye simu zaidi hata ya saa, yani unaongea na mademu story mpaka unakuja shangaa muda wote huo inakuaje .
Sasa kwet hao mademu wakali walikua wana kuja home sababu cousin wangu alikua ni rafiki zao, sasa mimi nilicho fanya simu ya chumbani kwa wazee, nika chomoa wire kwnye speaker , so inakua anaye ongea hasikii, so nikiona demu ana piga simu basi na mimi fasta chumbani , naipokea anaanza wasikiliza, dah .
Taarifa kwa mademu ,, Kama wewe ni demu na ulikua umekuja kwetu halafu ukaonega na bwana wako kwenye simu basi ujue nili kuwa nawasikiliza nina siri kibao za hawa warembo hahahahaa
 
Ndio maana nilikua simuoni na nilikua sija mjua kabisa ,sasa alikua ana hang wapi maana Coco ndio ilikuwa sehemu pekee ya wakishua , hivi ilkua ni wapi kwingine ?
Kuna mademu fulani nime wasahau walikua wana soma ITS ,mmoja laikua Mzambia na Mwingine Mganda, mmoja alini shobokea nika wan na hang naye halafu domo zito , tulikuwa tukienda kwao kwnye party reagent , sometime walikua wanakuja na gari ya baba yao Mercedez ya number za ubalozi , halafu mimi nikachemsha sababu alikua Mossy au Robert Byabato wako nao so close , ila demu aka shoboka kisiri na mimi , ila mimi kwa ujinga eti nikaogopa sababu washkaji ndio mademu zao , anyways nilikua domo zege kinamna, ila demu alinielewa, alikua anaitwa kitu kama Lilian or Joan , her lastname ndio tulikua tuna make fun of it , somebody Shipwashoke.
Alphonce kumbe alikuwepo miaka hiyo , duh , nakumbuka pale ilikuwa changing room ime choka kinoma, hapo ndio ilikua ina fanyika beach parties na umeme tuna chukua kw akina Kapere Shaba ,.
Ninasikia baadae bech parties zikaja kufungwa baada ya wimbi la wahuni toka Manzese walipo anza kuja hapo na kuona watoto wa kishua wako wamevaa mini skirts wakata mbaka binti ya mmoja wa mtoto wa mama moja alikuwa waziri na sikia akaokolewa na police na toka hapo Beach partis zika pigwa marufuku .
 
Halafu kuna jamaa fulani hivi , kipindi hicho kama walikua wana soma Tambaza au Azania, walikua brothers , walikua warefu sana , nadhani wali kwenda USA , tulikuwa tunambiwa eti walichoma sindano magotini eti wawe warefu, kitu kama walikua ni wamasai na walikaa Reagent or Mikocheni . kitu kama wali pata scholarship ya kwenda kucheza basktett ball , nani ana wa jua ni kina nani wale walikua?
 
Kumbe ni hao , aisee, nime kaa sana kule ndio maan nimewajua wengi, halafu kule karibu wote tulikua tunajuana ndio maana imekuwa rahisi kukumbukana , hahahahahahaha
Ofcoz zamani ilikuwa rahis kujuana coz community haikuwa kubwa na obay ilikuwa mitaa ya class fulani iliyojitenga tofauti na sasa hv ambapo imejaa watu wa aina tofauti so kujuana sio rahis coz community ishakuwa kubwa/population imeongezeka na eneo limekua la kibiashara zaidi
 
Wakati huo KGB ya Urusi ya zamani (USSR) ilikuwa ipo kazini, tena ilikuwa ipo active sana. Aidha, walikuwa wakitoa mafunzo k wa watu wa nchi nyingi sana duniani, Tanzania ikiwemo pia.
 
Taratibu na wewe utafunguka. Kumbe na wewe wa kishua atiiii. Si unaona ulisoma Forodhani shule za ushuani? So lots of memories to share……
ila mrangi Dar anaifahamu vema. Kila nikiona nyuzi kama hizi najua jamaa ataweka madini ya kutosha. kuna Uzi wa kuhusu mapedeshee wa mjini miaka hiyo….…..jamaa kautendea haki sana. Nimejifunza mengi. Big up sana mrangi kijana wa mjini…….
 
I can imagine hizo communities what they had in common ni wazee wao walikuwa na nafasi kubwa serikalini. Hivi hiyo miaka kulikuwa na non serikali people Obay na Masaki? I bet hata kama walikuwepo the likes of Mengi…….siyo wengi.
 
Sio mmoja alikuwa anaitwa Ipyana nadhani, tumecheza nao sana basketball kwenye half court ya Mzee Malay(rRIP) na kina Mazula, Warioba, halafu tulikuwa tunaenda kuomba mechi na watoto wa Masaki mwisho kina Mpoki(RIP), Eric Mwenda, daaah, zamani kweli mitaa ile tulikuwa tunajiona tunaishi US, mtu jua kali unavaa ki jumper cha hoodie
Tumeingia sana IST kucheza basketball na wototo wa kizungu
 
Aisee, umenikumbsha Mhalibwa Grocery, huyo Mtafungwa alikuwa anashinda Mhalibwa muda wote unamkuta pale
Tulikuwa tunakaa jirani na sana kina Ntuyabaliwe, wale madada wawili na mdogo wao, Jackline huyo kalikuwa katoto kadogo, mara nimeshaondoka bongo miaka kadhaa, unakuja kusikia ndio Miss Bongo, mara Mrs Mengi, sio Mchezo..
 
Duh, si mdingi alitukuta tunaangalia movie ya Pretty Woman, mbona tulitafutana nani kaleta hiyo movie nyumbani 🤣
Hizo Death Wish, basi Mdingi aliileta mwenyewe mbona ilizimiwa katikati, tukaenda kuzitafuta wenyewe na kuangalia zote mpaka ya Death Wish V
 

Bill ilikuwla inalipwa na serikali obviously maana hata security guards walikuwa wanalipwa na serikali. Mi nimeona bunduki live for the first time kwa mlinzi wetu alikuwa anaitwa Yessaya nakumbuka.
Tom amesoma na kaka yangu ambaye was two classes ahead of me. Mdogo wake mwenye kuvaa socks ndefu ndo nimesoma naye class moja yaani nachokumbuka kwake ni zile socks na the fact kuwa alikuwa mtoto wa mwalimu basi.
 
Anawachora tu wenzake. Hukumuzuku kasoma Shaban Robert na IST Kabla ya awamu ya pili ya Mzee Ruksa anakuaje si wakishua huyu. Hahahaaa.
 
Dah kweli ilikua longtime , aisee, nadhani ni yule mdogo anaye mfuatia sio yule mwingine ambaye alikua mdogo zado ndio ulizoma naye ,nakumbuka enzi zile hao kina Alpha walitufundisha utundu wa kupiga prank call police, basi tukawa tuna piga police halafu tuna kata , nadhani police walikua na technology kipindi hicho ya kujua call imepigwa toka eno gani ila na dhani walishindwa jua toka nyumba gani, maaba baada y amuda unaona Police hao wana pita nje na kigonra wakitafuta call imepigwa toka wapi, Enzi zile Police knye tukio ukipiga tuu wana kuja fasta, kulikuwa na ustaraabu sana , magari ya taka yana kujja , hivy mnatoa trash cans nje, kila jumamosi linapita tractor linakata majani , Unakumbuka like gari la Ice cream linapiga mziki , uklisikia a mile away unatoka mbio kulisubiri hapo ume sha piga mzinga mzazi ya aice cream, kibao housegirl wetu akawa ana tutusha ana tuambia ukienda peke yako yule drever ana kuteka, nika wan aogopa kalisogelea nikiw apeke yangu, kumbe dreveer na housgirl wan ajuana siku naona gari ime simama getini kwetu halafu haipigi mziki , nilitoka mbio nikidhani nimekuja tekwa hahahhahah
 
Kwani kamtaja Rizwan mkuu?!
Huoni kwamba ndio hawa wanao umia kuona watoto kufuata nyayo za baba zao , hawa ndio wan akesha kwnye mitandao kuponda ooh fulani kabebwa , sasa sijui walitaka watot wawe mafundi cherehani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…