Vifurushi vya intaneti 'visivyo rasmi' kwa kampuni za simu

6mbps mkuu unastream 1080p site zenye compression nzuri kama Youtube na Netflix, ama 720P site za kawaida.

Kama unatumia tu wewe mwenyewe sio mbaya, inategemea tu na bei.

TTCL ulikwama kabisa?
Lakini Mkuu dedicated si hata mkiwa 10 huwa haishuki speed?

TTCL miyeyusho mpaka ilifika muda hadi ofisi yao wote wakawa wananijua. Nikifika tu mlangoni kila mtu anasema "we jamaa bado tu swala lako mpala leo halijatatuliwa"

TTCL nimeachana nao kumbe kuna brother wa mtaa anapiga mishe za installation ya hizi internet kwenye moja ya kampuni ambazo zinatumia microwave.

Kaniambia atanifungia dedicated ya Mbps6
 
Pole sana mkuu, ulisumbuana nao kwa muda gani hawa wazee wa kumenoga?
 
maisha ya sasa kila kitu bei iko juu! Si vifurushi vya simu si ving'amuzi Inakoelekea hali itakua ngumu kwa watanzania wa hali ya chini!
 
Dedicated ina maanisha tu mda wote utapata 6mbps haimaanishi mkitumia watu wengi (Nyumba moja) speed haishuki.

Shared internet ina maanisha speed yako inaweza ikashuka ikiwa watu wengi wanatumia internet kwa wakati huo.

Chukulia mfano kampuni X imeleta Fiber 10Gbps capacity, wanaunga Vifurushi vya 10mbps kwenye Dedicated wataunga Exactly watu 1000 (1000x10mbps ni 10Gbps) ila kwenye Shared wanaweza wakaunga hata watu 5000 halafu mnagombania wenyewe hio bandwidth, assume siku kuna mechi kali kila mtu anatumia internet hapo ndio unaona speed inadrop toka 10mbps hadi 2mbps.

Pia mkuu most of time hizi internet za speed ndogo ni mtu wa kati, Mfano hio Microwave kuna possibility kubwa ni Vodacom supakasi, wapo pia wanaotumia za TTCL kisha wanauza rejareja.

TTCL tafuta fundi wa eneo husika, Sometime hakuna router tu hawaji kufungia watu, ukiongea nao unajua tatizo lipo wapi.
 
Chief-Mkwawa 5G coverage ya Airtel nayo ikoje, au ndo yale yale mpaka nikasimame posta mtaa fulani.
5G nyingi mkuu zina coverage ndogo sababu ya frequency kubwa wanazotumia,

Ukiangalia hizi data za mauzo ya frequency

Airtel 5G inaweza kuwa 2600mhz ama 3500mhz, hii 2600 angalau kuna ka uafadhali inaweza kuwa na coverage kubwa kidogo ila 3500mhz coverage ni ndogo na ndio wanatumia Voda na Tigo pia.

Hivyo kuna uwezekano mkubwa ikawa ni mjini tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…