I am Groot
JF-Expert Member
- Jul 20, 2018
- 3,929
- 10,747
Japan ni nchi inatotegemea exportation kwa kiasi kikubwa sana mbona thamani JPY ni ndogo.Nchi ikipunguza importation ya bidhaa na kuongeza exportation ya bidhaa zake automatically pesa yake itapanda thamani.
Kwa mfano TZ tukiwauzia Marekani mahindi, watatupa dollar hizo dollar zitaongezeka humu TZ na kusababisha thamani ya dollar kupungua humu TZ.
Dah! Swali zuri sana haya wajuvi mjibu hili swaliJapan ni nchi inatotegemea exportation kwa kiasi kikubwa sana mbona thamani JPY ni ndogo.
Ni ndogo ukilinganisha na ipi?Japan ni nchi inatotegemea exportation kwa kiasi kikubwa sana mbona thamani JPY ni ndogo.
Shilingi ya kenyaNi ndogo ukilinganisha na ipi?
Kumbuka Japan ipo nyuma ya China, marekani na ujerumani kwa nchi zinazo export sana.
Na pia kuna nchi nyingi zenye pesa yenye thamani kubwa kuliko hata marekani.
Factors zipo nyingi zenye kuchangia ukuaji wa thamani ya pesa
Maelezo mazuri bossMojawapo ya vigezo ni pale nchi inapozalisha kwa kiwango Cha juu Sana na kufanya udhaifu wa sarafu yako kuonekana Kama ndio "competitive edge" dhidi ya nchi washindani. Hapo hushauriwa kuongeza thamani ya sarafu.
Sababu nyingine ni uamuzi na utashi wa kisiasa hasa pale ambapo unakuwa muagizaji wa bidhaa nyingi kutoka nje kiasi Cha kuonekana sarafu yako kuserereka na huwezi kutumia njia ya kawaida ya demand and supply kuadjust.
Sababu nyingine inaweza kutokea automatic kutokana na sababu za kiuchumi. Kama vile tukikubali kufanya biashara za moja kwa moja Kati ya nchi mbili(bilateral trade) inayohusisha currency za nchi mbili,mfano Tz vs Malawi au Tz vs Burundi bila kupitia dola, basi inaweza kutokea sarafu ikajenga nguvu dhidi ya sarafu ya hiyo nchi nyingine kwa mfululizo wa muda mrefu na hivyo kuonekana kupanda thamani dhidi ya sarafu Fulani.
Kwa nchi inayozalisha na kuhitaji kuuza nje bidhaa zake kuliko nchi nyingine, basi huamua sarafu yake kuwa na thamani ndogo. Uimara wa sarafu ya nchi dhidi ya nchi nyingine haivutii ununuzi wa bidhaa za ndani ya nchi yako. Japan au China zikiimarisha sarafu zake, basi itasababisha wanunuzi kuhitaji dola nyingi (relatively) ili kuweza kununua bidhaa za nchi hizo kuliko ilivyo sawa na hivyo zaweza kupoteza wateja dhidi ya Marekani, Canada, EU, Australia, Africa na nchi zingine zinazopenda dola. Nani anataka kupoteza wateja?Japan ni nchi inatotegemea exportation kwa kiasi kikubwa sana mbona thamani JPY ni ndogo.