Vigezo gani hufuatwa duniani katika kuongeza thamani ya pesa ya nchi?

I am Groot

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2018
Posts
3,929
Reaction score
10,747
Wakuu,

Naomba kupata mwanga kidogo juu ya vigezo ambavyo nchi fulani duniani huchukuwa kuongeza thamani au pesa mpya katika mzunguko wa kiuchumi. Mfano, tuchukulie labda Tanzania hapa; inawezekana kuna kipindi kulikuwa hakuna pesa au noti ya shilingi 10,000 ila baadaye ilitambulishwa na kuanza kutumika.

Ni vigezo gani na hatua zipi zilifuatwa?
 
Mojawapo ya vigezo ni pale nchi inapozalisha kwa kiwango Cha juu Sana na kufanya udhaifu wa sarafu yako kuonekana Kama ndio "competitive edge" dhidi ya nchi washindani. Hapo hushauriwa kuongeza thamani ya sarafu.
Sababu nyingine ni uamuzi na utashi wa kisiasa hasa pale ambapo unakuwa muagizaji wa bidhaa nyingi kutoka nje kiasi Cha kuonekana sarafu yako kuserereka na huwezi kutumia njia ya kawaida ya demand and supply kuadjust.
Sababu nyingine inaweza kutokea automatic kutokana na sababu za kiuchumi. Kama vile tukikubali kufanya biashara za moja kwa moja Kati ya nchi mbili(bilateral trade) inayohusisha currency za nchi mbili,mfano Tz vs Malawi au Tz vs Burundi bila kupitia dola, basi inaweza kutokea sarafu ikajenga nguvu dhidi ya sarafu ya hiyo nchi nyingine kwa mfululizo wa muda mrefu na hivyo kuonekana kupanda thamani dhidi ya sarafu Fulani.
 
Forces za demand and supply ndio hupelekea thamani ya pesa kupanda au kushuka
 
Nchi ikipunguza importation ya bidhaa na kuongeza exportation ya bidhaa zake automatically pesa yake itapanda thamani.

Kwa mfano TZ tukiwauzia Marekani mahindi, watatupa dollar hizo dollar zitaongezeka humu TZ na kusababisha thamani ya dollar kupungua humu TZ.
 
Japan ni nchi inatotegemea exportation kwa kiasi kikubwa sana mbona thamani JPY ni ndogo.
 
Dah! Swali zuri sana haya wajuvi mjibu hili swali

Tena kuna mdau mmoja humu jukwaani alisema kenya pesa yao ipo juu kuliko japan hebu tupeni ufafanuzi juu ya haya mambo
 
Japan ni nchi inatotegemea exportation kwa kiasi kikubwa sana mbona thamani JPY ni ndogo.
Ni ndogo ukilinganisha na ipi?
Kumbuka Japan ipo nyuma ya China, marekani na ujerumani kwa nchi zinazo export sana.

Na pia kuna nchi nyingi zenye pesa yenye thamani kubwa kuliko hata marekani.

Factors zipo nyingi zenye kuchangia ukuaji wa thamani ya pesa
 
Shilingi ya kenya
1ksh = 1.07jpy
1jpy=0.12 zambian kwacha.

Kenya na zambia haziizidi jp kwa export, kwa nini hizo nchi mbili masikini zina sarafu yenye nguvu kuliko jpy.
 
Mojawapo ya vigezo ni pale nchi inapozalisha kwa kiwango Cha juu Sana na kufanya udhaifu wa sarafu yako kuonekana Kama ndio "competitive edge" dhidi ya nchi washindani. Hapo hushauriwa kuongeza thamani ya sarafu.
Sababu nyingine ni uamuzi na utashi wa kisiasa hasa pale ambapo unakuwa muagizaji wa bidhaa nyingi kutoka nje kiasi Cha kuonekana sarafu yako kuserereka na huwezi kutumia njia ya kawaida ya demand and supply kuadjust.
Sababu nyingine inaweza kutokea automatic kutokana na sababu za kiuchumi. Kama vile tukikubali kufanya biashara za moja kwa moja Kati ya nchi mbili(bilateral trade) inayohusisha currency za nchi mbili,mfano Tz vs Malawi au Tz vs Burundi bila kupitia dola, basi inaweza kutokea sarafu ikajenga nguvu dhidi ya sarafu ya hiyo nchi nyingine kwa mfululizo wa muda mrefu na hivyo kuonekana kupanda thamani dhidi ya sarafu Fulani.
Maelezo mazuri boss
 
Japan ni nchi inatotegemea exportation kwa kiasi kikubwa sana mbona thamani JPY ni ndogo.
Kwa nchi inayozalisha na kuhitaji kuuza nje bidhaa zake kuliko nchi nyingine, basi huamua sarafu yake kuwa na thamani ndogo. Uimara wa sarafu ya nchi dhidi ya nchi nyingine haivutii ununuzi wa bidhaa za ndani ya nchi yako. Japan au China zikiimarisha sarafu zake, basi itasababisha wanunuzi kuhitaji dola nyingi (relatively) ili kuweza kununua bidhaa za nchi hizo kuliko ilivyo sawa na hivyo zaweza kupoteza wateja dhidi ya Marekani, Canada, EU, Australia, Africa na nchi zingine zinazopenda dola. Nani anataka kupoteza wateja?
 
Sarafu za mashariki ya Kati ni imara sana (fuatilia) dhidi ya sarafu nyingi za nchi zingine. Sababu ukubwa hapa ni upatikanaji wa mafuta kwa wingi katika nchi zao. Nchi nyingi zinatoa sarafu zao kununua dola ili hizo dola zitumike kununua mafuta katika mataifa ya mashariki ya Kati. Mtu atauliza hapa, how about wao kununua magari, mitambo, silaha na bidhaa zingine kutoka Marekani,Japan, EU nk; Jibu la hapo ni kwamba wao hupata dola nyingi kutoka uuzaji wa mafuta na hivyo huwa na dola za kutosha na kubaki kununua bidhaa zingine nje ya nchi zao(balance of payment zinazohusisha dola ni positive).
 
Back
Top Bottom