Vigezo na masharti ya Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu vyawekwa hadharani

Vigezo na masharti ya Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu vyawekwa hadharani

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Mwenyekit wa kamati ya Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu, Prof. Penina Mlama, ametangaza vigezo vya kushiriki katika duru ya nne ya tuzo hiyo ya ya mwaka 2025/2026 yenye lengo la kukuza lugha ya Kiswahili na kuthamini mchango wa Mwalimu Nyerere.

Ameeleza hayo kwenye kikao na waandishi wa habari leo tarehe 13/8/2025 jijini Dar es salaam ambapo amewataka waandishi bunifu kujitokeza kwa wingi kuwasilisha miswada yao ambayo itaaanza kupokelewa tarehe 15/08/2025 hadi Novemba 30, 2025.
f1fcc425-b8af-4603-bf5a-88461beb4e06.jpeg

91472cc7-a40c-4c68-b8cc-26758107b16f.jpeg
“Sasa vigezo ndio hivyo tumevitaja ni wakati wenu waandishi bunifu kuweza kujitokeza kwa wingi kuwasilisha miswada yenu ili iweze kushindaniwa”amesema Prof. Mlama.

Vigezo mbalimbali vimetajwa vikiwemo Mshiriki awe raia wa Tanzania, andiko bunifu liwe katika lugha ya Kiswahili, Sehemu yoyote ya mswada isiwe imechapishwa na mchapishaji au kuchapishwa binafsi pamoja na kuchapishwa mtandaoni na magazetini, au kurushwa katika vyombo vya habari na burudani au kuoneshwa jukwaani.

Vigezo vingine ni pamoja na mwandishi anaruhusiwa kushiriki andiko bunifu moja tu katika nyanja atakayochagua, Mswada utakaoshinda tuzo nyingine hautazingatiwa, andiko bunifu litakalowasilishwa liwe andiko makini lililojikita katika masuala muhimu ya jamii.

Ameongeza kuwa miswada iliyoshika nafasi ya 1 - 10 katika tuzo ya miaka iliyopita haitaruhusiwa kushiriki lakini mwandishi anaweza kuleta mswada mwingine.

Kwa upande wake , Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) ambao ndio waratibu wa tuzo hiyo, Dkt. Aneth Komba, ameeleza kuwa uanzishwaji wa tuzo hiyo umesaidia sana katika uongezekaji wa machapisho bunifu yenye maadili ya kitanzania ambayo yanatumika kwa wanafunzi shuleni kujifunzia.
Screenshot 2025-08-13 190049.jpg

Screenshot 2025-08-13 190107.jpg
“Tunashukuru sana tuzo zimesaidia kukuza uandishi bunifu kwani kwa sasa machapisho yameongezeka ambayo sasa yana tamaduni za Kitanzania na yanatumuika kwa wanafunzi shuleni. Hili ni jambo kubwa kwa uanzishwaji wa tuzo hiyo”amesema Dkt. Komba.

Maadhimisho ya tuzo hiyo hufanyika kila tarehe 13 Aprili siku ya kuzaliwa kwa hayati Julius Kambarage Nyerere ambaye alifanya kazi kubwa ya kuenzi lugha ya kiswahili.


Vigezo hivyo ni kama ifuatavyo:

1. Mshiriki awe raia wa Tanzania.

2. Andiko bunifu liwe katika lugha ya Kiswahili.

3. Sehemu yoyote ya mswada isiwe imechapishwa na mchapishaji au kuchapishwa binafsi pamoja na kuchapishwa mtandaoni na magazetini, au kurushwa katika vyombo vya habari na burudani au kuoneshwa jukwaani.

4. Mwandishi anaruhusiwa kushiriki andiko bunifu moja tu katika nyanja atakayochagua.

5. Mswada utakaoshinda tuzo nyingine hautazingatiwa.

6. Andiko bunifu litakalowasilishwa liwe andiko makini lililojikita katika masuala muhimu ya jamii.

7. Miswada iliyoshika nafasi ya 1 - 10 katika tuzo ya miaka iliyopita haitaruhusiwa kushiriki. Hata hivyo, mwandishi anaweza kuleta mswada mwingine.
 
Back
Top Bottom