Vigezo vya kugombea ubunge , udiwani na urais viboreshwe, la sivyo tutatengeneza Taifa lenye viongozi vilaza

Vigezo vya kugombea ubunge , udiwani na urais viboreshwe, la sivyo tutatengeneza Taifa lenye viongozi vilaza

mshale21

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2021
Posts
2,517
Reaction score
6,074
Kwa vigezo vilivyopo na katiba mbovu tuliyonayo , ni wazi kabisa tunakoelekea tutatengeneza wabunge na mawaziri vilaza kuliko kawaida.

Nashauri hili suala liangaliwe kwa jisho la tatu na kwa wivu mkubwa kwa maslahi mapana ya taifa letu, ni wazi kabisa kuwa walioitengeneza katiba hii hawakukurupuka, yawezekana zama hizo wasomi walikuwa ni wachache ndiyo maana wakaweka kigezo cha kusoma na kuandika na elimu ya darasa la saba kuwa kigezo muhimu kugombea ubunge na udiwani.

lakini kwa karne hii , mwaka 2025 ambpo kumekuwa na wimbi la wasomi tele kwa kila idara, bado kigezo cha kuwania ubunge kiwe darasa la saba , kujua kusoma na kuandika kweli?

Yaaani mtu asiye na maarifa yoyote akashiriki kutenga sheria zinazoamua hatma ya watanzania na taifa kwa ujumla kweli?

Kwamba wanaachwa maprofesa, na madaktari wa taaluma mbalimbali kwenda kutunga sheria thabiti zinazoenda kusimamia maslahi mapana ya nchi yetu, badala yake wanapelekwa machawa kwa kigezo cha kujua kusoma na kuandika , yaani kazi yao ni kupiga makofi kwenye mbao za bunge kupitisha sheria mbovu?

Watanzania tubadilike, vigezo vya kugombea nafasi muhimu hizi vibadilishwe, ili tuepuke kuwapata watu kama Babu tale nk, nashauri nafasi ya ubunge angalau mtu awe na masters, udiwani angalau mtu awe na degree, TULIPE HADHI BUNGE NA TAIFA KWA UJUMLA
 
Back
Top Bottom