Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche akiwa kwenye picha ya pamoja na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA Godbless Lema, Makamu Mwenyekiti CHADEMA upande wa Zanzibar, Said Mzee; na Mwanasheria Mkuu wa chama hicho Dkt.Rugemeleza Nshala baada ya kikao kilichofanyika leo Septemba 17, 2026 jijini Dar es Salaam.
Viongozi hao wamekutana katikati ya uwepo wa madai ya kutuhumiana na kurushiana maneno baina ya viongozi na wanachama wa chama hicho ambayo yamekuwa yakionekana katika majukwaa ya mitandao ya kijamii, madai ambayo yamewahusisha pia wanaharakati, hivyo kikao hicho kimetajwa kuwa sehemu ya jitihada za kuimarisha Umoja na mshikamano ndani ya chama hicho kikuu cha upinzani nchini Tanzania.