Vigogo wa Chadema katika picha ya pamoja baada ya kikao cha leo

Magesi

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2012
Posts
2,600
Reaction score
624
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche akiwa kwenye picha ya pamoja na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA Godbless Lema, Makamu Mwenyekiti CHADEMA upande wa Zanzibar, Said Mzee; na Mwanasheria Mkuu wa chama hicho Dkt.Rugemeleza Nshala baada ya kikao kilichofanyika leo Septemba 17, 2026 jijini Dar es Salaam.

Viongozi hao wamekutana katikati ya uwepo wa madai ya kutuhumiana na kurushiana maneno baina ya viongozi na wanachama wa chama hicho ambayo yamekuwa yakionekana katika majukwaa ya mitandao ya kijamii, madai ambayo yamewahusisha pia wanaharakati, hivyo kikao hicho kimetajwa kuwa sehemu ya jitihada za kuimarisha Umoja na mshikamano ndani ya chama hicho kikuu cha upinzani nchini Tanzania.

 
Aliyelamba asali utamuona tu, mikono mfukoni, ile kiboss ariiiif...
 
Cdm sio chama kikuu cha upinzani Tanzania, bali ni chama kikuu cha siasa hapa Tanzania. Hiyo chama kikuu cha upinzani ni muongozo wa kiccm.
 
Lema kaiweka Chadema mfukoni. Alipotangaza tu kuwa atakuwa na Pres Conference, kila mwana Chadema alihaha hadi mnyea mtondoo Lissu akaagiza kwa namna yoyote Lema asifanye press conference. Akiifanya tu, mimi Lissu nanyongwa na Chadema inakufa! Ahahahahaha!!
 
CDM sio kama CCM ambalo Makamu wa Rais anafukuzwa kama mbwa na kupigwa biti asiongee kitu ajifungie ndani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…