Natumaini mko poa. Leo tena natumia haki yangu ya kikatiba kutoa maoni. Uzi huu unahusu vijana wanaoshangilia ushindi kabla mechi haijaisha. Ni kuwa kuna tabia ya wamiliki wa biashara ndogo kutofuata stages za ukuaji. Kama tunavyojua biashara ni kuhakikisha matumizi kidogo huku faida ikiwa kubwa (minimizing costs and maximising the profit). Nimeona vijana wengi wanajikuta mapema sana wanazidiwa na gharama za uendeshaji na kuingia kwenye matatizo sababu ikiwa wao wenyewe.
Biashara mwanzoni inahitaji uvumilivu na kujitoa sana kwa mmiliki wa hiyo biashara. Yaani pale mwanzoni mmiliki unatakiwa upigike haswa kabla ya kuongeza timu. Sasa hapa town utakuta dogo ndo anaanza biashara ila tayari kaweka secretary, meneja hadi mfanya usafi huku yeye akivimba balaa kama boss. Huu ujinga umewafanya wengi kushindwa mapema sana. Hizo gharama za mishahara utazilipaje? Vijana anza kumenyeka wewe mwenyewe kwa kiasi kikubwa na kadiri biashara inavyokuwa watu wataongezeka. Usilazimishe kuwa na watu wengi mwanzoni. Bana matumizi.
Pia wale wanaotumia pesa kufanya decorations za ofisi mjikumbushe huu uzi.
www.jamiiforums.com

Vijana acheni kuwekeza sana kwenye decorations za duka badala ya stock
Mojawapo ya kosa kubwa sana la kiufundi kwa vijana wengi wadogo wanaoanza biashara ni kuwekeza pesa nyingi kwenye vitu ambavyo havirudishi pesa kwa haraka au pengine havirudishi kabisa. Vijana wanafungua maduka ila wengie hawafikishi mwaka mmoja wamefunga baada ya kushindwa biashara. Vijana...