Magonjwa yasiyo ya kuambukizwa mfano moyo, kiasukari presha na saratani yanakua na risk factors nyingi ikiwemo
👉Umri
👉mtindo wa maisha
👉Genetics
Na tunajua risk factors sio chanzo cha moja kwa moja bali ni mambo ambayo ukiyafanya yanaweza kukuelekea ukapata magonjwa hayo
Mtu anaweza asiwe na umri mkubwa na mtindo wake wa maisha ni wa kawaida sio sedentary lifestyle, anapiga zoezi vizuri lakini akapata kisukari akapata pia saratani na hata (
cardiac diseases) juzi tu tumesolve kesi moja mtoto wa miaka miwili ana myocardial infraction. Ila anaendelea vema
Hapo kuna factor moja imebaki ambayo ni genetics.
Kuhusu energy drinks na kuleta magonjwa ya moyo probably inaweza sababisha lakini inaingia hapo kwenye mtindo wa maisha.
Energy drink ni kwaajili ya kupunguza fatigue ikiwa kuna ulazima wa kuendelea kufanya kazi na ingredient yake kubwa ni caffeine, ambayo pia unaipata kwenye kahawa na alkaloids zingine. (kwa waliokutana na pharmacognosy wataelewa nini namaanisha )ikitumiwa kiasi sidhani kama inaweza leta ugonjwa wa moyo, na tunajua too much is harmful.
Hapo juu nimeona kuna member anakunywa energy 6 kwa siku
Wanachuo wanakunywa energy na skonzi😂 hio ndio chai pia mtu anakunywa energy drink kisha anaenda kulala😂😂 for what?
Kwa staili hio tutapona kweli?
All in all too much is harmful
Dkt. Gwajima D
Dr Restart
DR Mambo Jambo
Dr am 4 real PhD
Mnaweza ongeza jambo hapa.