Vijana acheni pombe na Energy drinks, mwifwa

Watoe maelezo kitaalamu hizo energy drink zina chemical zipi ndani yake zinaopelekea kuharibu figo, sio kusema tu energy drinks zinaharibu figo.
Hii itasaidia sana watu wapate uelewa kwa upana zaidi.
Mkuu fegi tu yenyewe imeandikwa uvutaji wa sigara ni hatari kwa afya yako na watu bado wanakula mwenge vibaya sana.

Sidhani kama wakiandika itasaidia chochote, solution wapige stop za kwenye chupa ya plastic waweke kwenye aluminium automatically na bei lazima ibadilike itapunguza sana matumizi yake.
 
Kwenye list Yako,toa nguluwe
 
Energy nakubaluana kabisa,nilikuwa mlevi wa Energy tena nilikuwa napenda lile la Mo kwakuwa kubwa,aisee nikaanza kidalili cha moyo kulipuka,wala sikuenda hospital nikasema hii ni energy tu,nilivyoacha nikawa safi kabisa.Nakaa mwaka hata Energy siitumi,kwa sababu haina faida yeyote
 
Sikuizi hizo pombe wanapima kwa vizibo.
Tabu iko palepale.
 
Pombe kali zina athari kubwa kwenye mwili, hasa ini lako.

Ini ni kiungo muhimu kinachosaidia kutoa sumu mwilini, lakini pombe kali zinaweza kuharibu ini yako.

Pia, kuna hatari ya magonjwa ya akili kama kuharibika kwa ubongo kwa sababu pombe inaathiri sehemu za ubongo zinazohusika na kumbukumbu na uamuzi.
 
Wacha wafe mkuu
 
Bahati mbaya ni kwamba watu wengi tunakujaga kijifunza na somo linaeleweka ukiwa umeshapatwa na shida.

Tunajifunza tukiwa tumeshachelewa, "Neno ningejua huja mwisho wa safari"

Uraibu wa hivi vitu ni mbaya... Kama kuna mtu bado ananafasi anajitambua basi namshuari apambane aache au jitahidi usije kutumia madawa ya kulevya hasa hasa pombe kali(pombe kali haizungumziwi lakini inaondoka na ndoto malengo/dira na hata uhai wa vijana wengi sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…