Vijana angalieni fursa hii

Yapo mazao kibao sio complicated na yana pesa ndefu. Eti mtu unahangaika na sijui mahindi, sijui mpunga. Lima mazao yenye uhakika wa kuvuna, ambayo hata wachawi hawashughuliki nayo kuyaloga
Korosho wanaroga sana
 
Kahtan Ahmed

MA SHAA ALLAH
HAADHA MIN FAADHIL RABBY
Kama ulichosema nikweli
Mabrouq..Kiongozi 👏

Nina maswali mengi kwako..naomba kujua haya yatuatayo..!!!

Maandalizi ya Shamba lako ulitumia Gharama kiasi gani kwenye kuliandaa? Kabla ya kuotesha? I mean kuanzia kufyeka Pori? Kutoa magugu? Na Parizi ni sh ngap?

Gharama za mbegu kwa hekari 1 ni sh ngap?

Gharama za uoteshaji kwa hao Vibarua/Cheap labours ni sh ngap kwa hekari 1?

Palizi baada ya kuotesha mbegu gharama zake ni sh ngap kwa heka?

Palizi inafanyika kila baada ya mda gani?

Umelima wapi eneo lako liko Wilaya gani uko Kusini?

Gharama za Usafiri kutoka Dar mpaka ulikolima izo Korosho ni sh ngap kwa bus?

Lodge za uko self contained/zenye choo ndani kwa usiku mmoja ni sh ngap?

Gharama za chakula ni sh ngap?

Lilipo Shamba na maeneo ya Lodge Sehemu ya Malazi ni Sh ngap kwa usafiri Maarufu wa Bodaboda?

Umekutana na changamoto gani kabla ya kuotesha na baada ya kuotesha?

Uliwezaje kutatua changamoto ulizokutana nazo ndani ya hiyo miaka 4?

Ndani ya hiyo miaka 4 ulitumia Gharama ya Sh ngap kabla ya mavuno?

Samahani kwa Maswali mengi naomba unijibu Kiongozi kwa faida ya wengi 🙏
 
Hapa Tanzania ndio blessed country among blessed countries.
Kigoma Kuna chikichi na Korosho na ardh ipo
Dodoma Kuna zabibu na ardhi iipo
Nyanda za juu kusini Kuna Parachichi na ardhi ipo
Kusini Kuna Korosho na ardhi ipo
Morogoro Kuna machungwa maembe na ardh ipo
Tanga Kuna matunda na ardhi ipo
Morogoro Kuna mkonge na ardhi ipo
Morogoro Kuna mitiki na ardhi ipo
Njombe Kuna miti ya mbao na ardhi ipo
Moshi Kuna ndizi ardhi adimu
Bukoba Kuna ndizi na ardhi sijui
Rungwe Kuna ndizi ardhi sio kubwa.
Pwani Kuna minazi na machungwa na ardhi ipo.
It only need time risk, focus and persistance.
Waache waendelee kzurura na mikanda, mitumba nk huku utajiri wameuacha kijini kwao.
 
Dah! kwa maswali haya, Bora uwepo ndani ya chumba cha mtihani Kuna nafuu kidogo kuliko kujibu maswali haya, maana hata ukimpa wiki 2 nahisi hatamaliza kujibu,ila ujasiliamali ni zaidi ya mtu kuonekana mwehu,asiye na maarifa,muongo Mmoja hivi n,k, jambo la muhimu wewe shikilia hayo maono yako wasikutoe kwenye mstari, yaani wasikukatishe tamaa ,Nina mengi ila kwa bahati sio muandishi mzuri
 
nimeshajibu maswali haya soma comment
 
nimefanya hivo pia mwaka juzi. nilinunua shamba eka 14. huko nanjilinji kwa sh 1.2m. nikapanda mikorosho. tatizo ni nyani nyani nyani. sijui wana shida gani wale wadudu. wanang'oa ile miti. mpaka sasa shamba halina hata mmea

Sio nyani watu hao mkuu...?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…