Vijana angalieni fursa hii

Vijana angalieni fursa hii

Leo ningependa kuwapa zawadi vijana wenzangu watizame hii fursa watakuja kunishukuru badae

Tatizo la vijana tulio wengi ni kuharakia maisha tunapenda kupata leo leo, jambo ambalo linapelekea kua na maisha magumu sana kila siku na tunaishia kufa maskini

Niwachache sanna wanaofanikiwa kwa shortcut na shortcut zinatugharimu sanna kwanini usitumie hii fursa

Maeneo ya kusini heka kumi nimenunua kwa million 1 tu

Nilichofanya nimesafisha shamba na kupanda mikorosho 490

Kisha nikawakatia vipande wana kijiji nikawambia limeni eneo hili bure kwa lengo la kulinda mikorosho

mwaka jana ndio ilikua mwaka wa nne tangu nipande mikorosho, nimekwenda kuvuna korosho tani 17 na nikauza kwa bei ya elf 1500 kuwauzia serikali ambao hua na maghala ya kununua korosho karibu na shamba langu la mikorosho nimelipwa mil 25

Nimewaza sanna tunahangaika na kutaka kukaa mjini tu ila fursa zipo na zipo nyingi zinazofanana na hizi
Asanteni
Barikiwa mkuu kwa kushare nasi hii: But nawakumbusha wadau kuwa Kila kitu hapa dunia kinaweza kufaa kukupa faida, LAKINI si kila kitu kimstahili kila mtu kumpa faida.. (Mkumbo ni shimo la hasara)..
 
Korosho zao la kisiasa madalali wengi kuliko wakulima wenyewe bora ungepanda mitu ata benk wangekupa mkopo mkuu kama una hati ya kimila lakini korosho mwaka huu kilo Shiling 980,
 
Mkuu mkorosho tangu kupandwa hadi kuvunwa inachukua miaka mingapi
 
Kwa kua umeamua kutupa dili basi fafanua vizuri ili tujue tunaanzia wapi,
Shamba umesema Milion 1
Mbegu?
Mbolea?
Palizi?
Dawa?
Muda wa kupanda?
Muda wa Mavuno?
Tupe mchanganuo mzuri tujiandae.
Swali zuri hili
 
wakatishe tamaa vijaa wenzio hali ya kua hukusema uongo upo wapi toa ushahidi kua nilichokiongea ni uongo
Fafanua vizuri ulifanyajefanyaje maana hauupandi tu mkorosho alafu ukasubiri mavuno baada ya mwaka au miaka 2, kuna gharama zingine haujazitaja hapa
 
Back
Top Bottom