Vijana Hatujazoea Kulalamika, Lakini Haya Yanayotokea Sasa Ni Beyond Uvumilivu!

Prof_Adventure_guide

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2023
Posts
533
Reaction score
1,499
Jamani wana JF, kuna jambo linaniumiza sana na natamani tulijadili kwa uwazi bila kuogopa. Kila siku tumekuwa tukisikia kauli zinazotuambia, “Vijana fanyeni kazi, acheni kulalamika.” Sawa, lakini mnataka kuniambia kweli vijana wa taifa hili hawafanyi kazi?

Ukweli ni kwamba vijana tumepitia vyuo, tumepambana kupata elimu, lakini kwa makusudi kabisa tumenyimwa ajira kwa miaka mingi. Pamoja na hayo hatukukata tamaa; tukaambiwa tujiajiri, tukakubali, tukanyanyuka, tukaanza biashara zetu kwa nguvu zotehatujawahi hata kuhusisha siasa wala kusukumwa na hisia za kisera.

Lakini sasa kinachotokea kinafika hatua ya kutuvunja moyo kabisa. Vijana tumekaa kimya kwa miaka mingi, tumefanya kazi, tumebeba majukumu ya familia, tumekuwa resilient kuliko inavyotarajiwa. Vyeti vya watu vimekaa ndani tangu enzi za Kikwete mpaka leo na bado tumenyamaza, tumepiga kazi tu.

Changamoto inakuja pale ambapo serikali hiyo hiyo inayotuambia “jiajirini” ndiyo inatuletea mzigo mkubwa wa kodi na tozo, kila kona unakutana na:

Leseni za biashara zisizoisha

Service levies

Tozo za kila mamlaka inayopita mitaani

Regulatory fees ambazo hazieleweki zimetoka wapi

Marekebisho ya ushuru kila mwaka bila maelezo ya msingi

Sasa mtu kama mimi, kijana niliyekataa kukaa bure, nikajipambania kuanzisha biashara, naambiwa nifanye kazi lakini wakati huo huo nanyongwa na kodi, tozo, na regulations ambazo hazina uhalisia wa ground.

Wanataka nishi vipi?
Wanataka niendeshe biashara vipi?
Wanataka nimsaidie familia vipi wakati kila hatua ninayojaribu kupiga inakatwa miguu?

Serikali inaposema “jiajirini,” inapaswa angalau kuweka mazingira ambayo yanamwacha kijana aweze kupumua, aweze kukua, aweze kuona mwanga wa kesho. Lakini badala yake, kinachotolewa ni pressure, stress, makato, na barriers zisizoisha. Inakuwa ni kama vijana tumewekwa kwenye “system ya kuteseka kimya kimya.”

Halafu waje kutegemea vijana wasiongee?
Jamani, this is not sustainable.
Hii sio sawa hata kidogo.

Wito wangu: sio kwamba vijana hatufanyi kazi—TUNAFANYA KAZI MORE THAN EVER, lakini tunahitaji ecosystem ambayo haikatishi tamaa, ambayo haipigi wananchi viboko vya kiuchumi halafu inawaambia wabaki watulivu.

Ndio maana watu wanaongea.
Na kwa kweli, kwa hali ilivyo sasa, kupaza sauti sio kulalamika ni self-defense ya maisha na future yetu.
 
HAYA NDO MAWAZO CHANYA...
SAFI KABISAA..

KATIKA HILI, KUNA HAJA YA KUBEBA YOTE ULIYOYAANDIKA MAANA HAKUNA TUSI, WALA KEJELI, BALI UMEONGEA UKWELI!
 
Tukomae tu hivi hivi Nyumbani ni Nyumbani hata kama hakupikwi chai
 
Back
Top Bottom