Uchaguzi 2020 Vijana hawana cha kupoteza kwa Dkt. John Pombe Magufuli

Uchaguzi 2020 Vijana hawana cha kupoteza kwa Dkt. John Pombe Magufuli

Sasa upinzani na mataahira ya Lumumba wapi kuliko na vijana wengi?
Usije ukadhania vijana wote ni Bavicha....kuna vijana wengi wazalendo hawana vyama ila wanajua utendaji kazi wa Mzalendo JPM na ndio watakaompa kura za kishindo.

October 28th kura zote za ndio ni kwa JPM

JPM ANATOSHA
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
 
Yani mimi kama kijana naisubiri sana hiyo tarehe 28 october tukawaonyeshe watanzania jinsi magufuli tunavyompenda vijana ...Yani kura zote kwa Dk John Magufuli....huyu mzee jamani katufanyia maendeleo mengi anaebisha kuna nati za kichwa zimechomoka

Una mimba ya kupitia haja kubwa!!Mambo gani makubwa ,?Vijana hawana ajira,maisha magumu mitaani,hakuna nyongeza ya mishahara!Ameua watu wengi!Mimi na mkoa wangu wa Mtwara kura zote kwa LISSU
 
Kwahiyo umejiunga mwezi uliopita ili uje utapike makande yaliyochacha huku jukwaani?
*UKWELI KUHUSU VITAMBULISHO VYA WAJASIRIAMALI*

Tangu kuanza kwa kampeni za Uchaguzi Mkuu, baadhi ya wagombea katika harakati za kushawishi wapiga kura, wameibuka na hoja ya vitambulisho vya wajasiriamali.
Hoja yao ni uhalali wa vitambulisho hivyo na umuhimu wake kwa wajasiriamali, wakidai kwamba vitambulisho hivi vina mapungufu mengi.

Katika kujenga hoja zao wanasema, vitambulisho hivi mosi, havina jina la mhusika wala picha yake, havionyeshi makazi, havionyeshi shughuli ya mhusika na havina saini ya mhusika.
Pili, wanadai gharama ya Sh. 20,000 ni kubwa sana kwa mjasiriamali wakitanzania.

Hoja hizi zimenifanya niamini mambo mawili, moja ni kwamba wanaotoa hoja hivi hawajafanya utafiti vizuri na kujua ukweli kuhusu vitambulisho hivi.
Lakini pia yawezekana kabisa wanaujua ukweli lakini wameamua kupotosha umma kwa maslahi yao ya kisiasa.

Kama Mtanzania mpenda maendeleo nimeona nisikae kimya, nitumie nafasi hii kueleza machache ninayoyajua kuhusu vitambulisho vya wajasiriamali, tukianza na sababu ya kuanzishwa kwake na utaratibu wanaopitia wajasiriamali hadi kuvipata.

*UANZISHWAJI WAKE*
Vitambulisho vya wajasiriamali vilianzishwa Desemba 10, 2018 na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli ili kuwasaidia wafanyabiashara wadogo kutambulika na waweze kufanya biashara zao kwa uhuru popote ndani ya Tanzania bila kubugudhiwa na yeyote kama ilivyokuwa awali.
Lengo lingine ni kuwawezesha wafanya biashara wadogo kushiriki kulijenga Taifa lao kwa kuchagia pato la taifa kwa kiasi hicho kidogo kwa mwaka, pesa ambayo Serikali inaitumia katika shughuli za kimaendeleo kama vile ujenzi na uboreshaji wa masoko, ujenzi wa vituo vya afya nk.

Kabla ya kuanzishwa kwa utaratibu wa vitambulisho hivi, wajasiriamali hawa walikuwa wakitozwa Sh.500 hadi Sh.2,000 ama zaidi kila siku ndipo waweze kufanya biashara.
Mjasiriamali aliyekuwa akilipa Sh.500 kwa siku, kwa mwaka alitumia Sh Sh.182,500 na aliyekuwa akilipa Sh.2,000 alijikuta akilipia Sh.730,000 kama tozo ya kufanya biashara eneo husika.
Ukiangalia Sh 20,000 inayolipwa na wajasiriamali kwa mwaka, ni kiwango kidogo sana ambacho ni sawa na Sh 55 tu kwa siku, huku pia mjasiriamali huyu akiwa na uhuru wa kufanya biashara popote pale.

*UTARATIBU WA KUPATA VITAMBULISHO*
Mchakato wa kupata vitambulisho hivi unaanzia kwenye ngazi ya chini kabisa ya kijiji/mitaa na kata.
Mjasiriamali atatakiwa kujaza fomu maalum ambapo taarifa zake muhimu kama vile majina kamili, umri wake, jinsia, eneo analotoka, picha pamoja na aina ya biashara anayofanya zitachukuliwa.
Pia mjasiriamali atatakiwa kuwasilisha kitambulisho kimojawapo kati ya vitambulisho vifuatavyo;
(i) Kitambulisho cha Taifa
(ii) Hati ya kusafiria
(iii) Leseni ya udereva
(iv) Barua ya utambulisho toka kwa Mtendaji wa Kata.

Kopi ya kitambulisho na taarifa zote muhimu za mjasiriamali zinabaki na kuhifadhiwa kwenye mifumo ya kieletroniki ambayo iko mahususi kwaajili ya kuhifadhi kanzi data ya wajasiriamali.
Baada ya hapo mjasiriamali atatakiwa kulipia Sh.20,000 tu kwa njia ya mifumo ya kielektroniki kama tozo ya mwaka mzima.
Baada ya utaratibu huo kukamilika mjasiriamali atakuwa amekidhi vigezo vya kupata kitambulisho hiki.
Kitambulisho hiki kinamtambulisha mjasiriamali kwa namba maalumu ambayo haijirudii kwa mjasiriamali mwingine yeyote.
Kwa ambao walikuwa bado hawafahamu vitambulisho hivi vya wajasiriamali vina taarifa zote muhimu kuhusu mjasiriamali husika aliyepewa kitambulisho hicho na kumfanya kutambulika popote atakapokuwepo ndani Tanzania, ni kama mfano wa usajili wa line za simu ambapo unachukuliwa taarifa zako zote muhimu.
Hata ikatokea kwa mfano mfanyabiashara mwenye kitambulisho namba 500 ambaye alisajiliwa Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa, akaenda kufanya uhalifu mkoani Mwanza na katika tukio hilo akakidondosha kitambulisho chake, kupitia ile namba tu ya kitambulisho atatambulika huyu ni mtu fulani kutoka eneo fulani na anafanya biashara fulani.
Kwa muktadha huu hoja ya kuwa vitambulisho hivi havina sifa na havimtambulishi mhusika inakosa mashiko lakini tukubaliane kuwa hata Roma haikujegwa kwa siku moja kikubwa tujikite kuona lengo la uashishwaji wake na faida ambazo watanzania wenzetu wajasiriamali wamezipata kupitia vitambulisho hivi na ikiwa huu ni mwaka wa pili tu toka kuanzishwa kwa vitambulisho hivi na kumekuwa na maboresho kutoka vitambulisho vya mwaka wa kwanza na mwaka uliofuata.
Naamini kama kutakuwa na ulazima au umuhimu wa maboresho mengine yatafanyika kulingana na uhitaji wa wakati.

Kwa leo nilipenda nieleze kwa uchache tu kuhusu uhalali wa vitambulisho hivi na faida yake kwa wajasiriamali ambao wengi wao ni mashahidi wa namna ambavyo vitambulisho hivi vimekuwa mkombozi kwao.
Wakati mwingine panapo majaaliwa nitaelezea kwa kina umuhimu wa vitambulisho hivi kwa wajasiriamali katika kuboresha biashara zao ikiwemo upatikanaji wa mikopo katika taasisi za kiserikali (mikopo isiyo na riba) na taasisi za kifedha kama ambavyo halmashauri ya Kigamboni kwa kushirikiana na Benki ya CRDB wameanza mchakato wa kutoa mikopo kwa wajasiriamali hawa maarufu kama
“Machinga Loans”

HAYA SEMA NA HIII NI MAKANDE SASA.
 
Hivi Lumumba mkishapewa t-shirt na kofia mnajionaga mna akili kuliko watanzania wengine na wamiliki wa hii nchi sio?
Hapa ndio nimegundua kua kuna haja ya wewe kufanyiwa upasuaji mdogo ili mishipa ya faham na akili ikae sawa.

SIO makosa yako
 
Kwahiyo umejiunga mwezi uliopita ili uje utapike makande yaliyochacha huku jukwaani?
Wewe ni fala tatizo lako, sasa unapata wapi uhalali wa kumhoji mtu saa,siku,mwezi na mwaka aliojiunga JF. Kama ni hivyo si ungepita kushoto usingejibu hoja yangu. Njia pekee ya kuhoji mtu ni kwa hoja zake na sio id yake.
 
Tunaanzaje kupoteza hakika katika hili maana Mh Rais Magufuli kafanya mengi kuliko hata yale ambayo tulikuwa tunatarajia kuyaona japo wapo watu wa ufipa wao kazi yao ni kupinga tu.
Hapohapo nashangaa wajomba bado mnatumia majimambo hayo ambayo Magufuli kayafanya maana duuuh nii hatari.
Mi naona tuanze utaratibu kwamba kwa anayepinga miradi na maendeleo basi wasiruhisiwe kutumia miradi na miundombinu yoyote iliyofanywa na Serikali
 
Mambo hayooooo
 

Attachments

  • IMG_20201017_182609.jpg
    IMG_20201017_182609.jpg
    19 KB · Views: 2
Tunaanzaje kupoteza hakika katika hili maana Mh Rais Magufuli kafanya mengi kuliko hata yale ambayo tulikuwa tunatarajia kuyaona japo wapo watu wa ufipa wao kazi yao ni kupinga tu.
Hapohapo nashangaa wajomba bado mnatumia majimambo hayo ambayo Magufuli kayafanya maana duuuh nii hatari.
Mi naona tuanze utaratibu kwamba kwa anayepinga miradi na maendeleo basi wasiruhisiwe kutumia miradi na miundombinu yoyote iliyofanywa na Serikali

Ni kweli kabisa, ili mradi msikusanye kodi kwetu, kisha muone sisi tutafanya nini kwa kodi zetu.
 
Back
Top Bottom