Vijana, inapaswa kumuiga huyu mzee Mkenya ambaye sifa zake zimeenea ulimwengu wote

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
32,408
Reaction score
50,809
Kwa kweli kuna wakati serikali zetu huzingua pale zinatelekeza majukumu, ikiwemo hii serikali yetu ya Kenya, na ni kawaida ya sisi sote kujawa na lawama, lakini nahisi ni muhimu kwa baadhi yetu kuchukua hatua na kufanya baadhi ya mambo wenyewe.

Sifa za huyu mzee zinazidi kuzagaa dunia yote, anatajwa kila mahali na ikiendelea hivi anaweza akatunukiwa tuzo la kimataifa.

Alichokifanya, baada ya kuona serikali ya mtaa imefumbia macho masaibu ya wanakijiji, ambao walikua wanateseka kwa ukosefu wa barabara, alinyanyua jembe na kuamua kuchimba mwenyewe.

Hivyo kwa vijana ambao kutwa ni lawama na kuvaa milegezo mjini wakishinda kwenye pool table, kuna la kujifunza hapa.

 
Alitunukiwa Ng'ombe wa Maziwa Aina ya Freshian anayekamuliwa lita arobaine kila siku. Hongera kwake.
 
Hongera Kwa Moyo alionao.
Mimi nalipa kodi nyingi sana, Siwezi fanya hiyo kazi aisee,
Yaani ni Sawa na Kumlipa kibarua akulimie shamba halafu unaenda kulima mwenyewe. Big No.
 
Hongera Kwa Moyo alionao.
Mimi nalipa kodi nyingi sana, Siwezi fanya hiyo kazi aisee,
Yaani ni Sawa na Kumlipa kibarua akulimie shamba halafu unaenda kulima mwenyewe. Big No.

Sio lazima unyanyue jembe ukachimbe barabarani, sio lazima ufanye alichokifanya, ila hapo ulipo una kitu unachoweza kukifanya kwenye level yako. Kwa mfano tu, unaweza kuwapa baadhi ya madogo mtaani elimu inayohusiana na utaalam wako, japo ni jukumu la serikali kwa kutumia kodi yako kuwaelimisha. Fanya mentoring kwa vijana au hata kijana mmoja bila kutegemea malipo yoyote, hakikisha kabla hujazikwa, humu duniani kuna vijana kadhaa ambao umeacha wakiendeleza jamii kwa juhudi zako mwenyewe.

Hakuna kitu hunipa fahari kama kuona nimemfanyia mentoring ya kitaalam dogo mpaka anakuja kuoa na kuendelea na maisha.

Tukiishi kwa mtazamo wa kutegemea serikali ifanye kila kitu kisa tunalipa kodi, tutabaki nyuma miaka yote, mji unakua mchafu kila mtu anatupa taka kote eti serikali iwatume watu waje wazoe maana tunawalipa kwa kodi.
 
Taarifa inakaribia miezi sita leo timu Tanga Tanga umeamka na hii zilipendwa story. Anyway anastahili pongezi
 
Taarifa inakaribia miezi sita leo timu Tanga Tanga umeamka na hii zilipendwa story. Anyway anastahili pongezi
Nafahamu ni taarifa ya zamani na kuna kipindi tuliijadli humu, ila leo nimeileta upya baada ya kuona imepokelewa hadi na ktuo changu pendwa cha YouTube kinachoitwa FV
 
Hongera Kwa Moyo alionao.
Mimi nalipa kodi nyingi sana, Siwezi fanya hiyo kazi aisee,
Yaani ni Sawa na Kumlipa kibarua akulimie shamba halafu unaenda kulima mwenyewe. Big No.
Danganyikan mentality hio, hutavuka pande ile nyingine ya mto hadi pale Serikali yako itajenga daraja???
 
Nimerudia kusoma ujumbe wako mara kadhaa.Umeandika kwa hisia sana..ngozi nyeusi kutoana ni nadra sana.Maelezo yako yanajitosheleza sana.

Nilikutana na boda boda mmoja mwaka 2016,alinisimulia jambo moja ambalo alikuwa akimsifia sana boss wake aliyempa boda boda.Alisema kuwa mpaka pale alipokuwa amenibeba amepata pikipiki mbili za kwake.Kijana yule alinibeba ilikuwa saa kumi alfajiri.Alijiamini sana na kazi yake,usafi na utulivu mkubwa barabarani..alizidi kusema zaidi,baada ya kumaliza form 4 na sina uelekeo alikuja bro mtaani kwetu anatafuta vijana wa kumsaidia na boda boda zake mbili.

Waliingia mkataba kuwa baada ya faida basi angebaki na boda boda.Kijana anasema utofauti wa boss wao ndio uliomfanya aheshimu sana ile kazi na kujiheshimu pia.Kwa sasa ni mtu mwenye mafanikio mazuri kwa kipato chake cha kati ambacho kimemsaidia kujiendeleza kupitia hiyo njia.

Uaminifu na kujiheshimu ni kitu muhimu sana kwa sisi vijana na watu wote.Kuthamini vitu vidogo vidogo huleta mafanikio makubwa sana katika maisha yetu.
 
Vijijini huko mbona ni mambo ya kawaida sana tena ina jina inaitwa "msaragambo" Nyerere ndio alianzisha huo utaratibu na saivi umeendelea kiasi cha wananchi kuchanga pesa na kujenga mpaka barabara za lami.

 
Danganyikan mentality hio, hutavuka pande ile nyingine ya mto hadi pale Serikali yako itajenga daraja???
Kwa Taarifa yako Tanzania shule za secondary maarufu kama "shule za kata" nchi nzima 70% zimejengwa na wananchi wenyewe kwa gharama zao kuanzia kutoa ardhi mpaka finishing

Hayo ni maelfu ya shule sio kijibarara.
 
Hope huu ujumbe ni kwa Wakenya wenzako na sio Watanzania

Watanzania watakushangaza zaidi 👇👇👇
Na hii ndio dhana halisi ya UJAMAA
 

Punguza mihemko uelewe Vizuri, Leo umenena maneno kuntu,
Nami nakubaliana nawe, mimi hufanya walau pale napopata nafasi hasa kukaa na vijana, Nakumbuka siku kadhaa zilizopita tumeenda kusafisha coco beach nilipata jukumu la kuongoza kundi la wanafunzi toka shule moja hapa dar kusafisha ufukwe Ilikuwa ni wasaha mzuri sana kwangu kuzungumza na Wanafunzi since I shifted to dar for my career,

I can do charity when I see the need, nakumbuka nilijitolea kufundisha sayansi wanafunzi wa Sekondari kabla na baada ya masomo ya elimu ya juu na hadi leo wengine wako vyuo vikuu na wengine wameajiriwa, kule kwetu kuna watu wanajua mimi ni Mwalimu hadi leo.
Hapo kwenye kujitolea kwa namna hiyo I agree with you, But Siwezi fanya kazi ya kutengeneza Barabara msee,

That’s Government Job, na mtu akitokea anisemeshe juu ya hili tutagombana kwakweli. Nalipa kodi nyingi sana huwa nikiangalia slip yangu na nikiangalia vile wanasiasa wanabehave roho inaniuma sana.
 
Vijijini huko mbona ni mambo ya kawaida sana tena ina jina inaitwa "msaragambo" Nyerere ndio alianzisha huo utaratibu na saivi umeendelea kiasi cha wananchi kuchanga pesa na kujenga mpaka barabara za lami.


Wacha kukurupuka kwa kuleta ligi, haya ni mambo tunayafanya sana vijijini, watu kuungana kwa pamoja na kufanya shughuli kama hii, ila maudhui ya huu uzi ni kuhusu mtu mmoja kutokuendela kusubiri serikali au jamii, kaamua mwenyewe kuchukua hatua.
Mfano mwengine huko Tanzania ni zile taarifa za mwalimu kujitolea kufundisha darasa lenye watoto 216 baada ya waalimu kukosekana https://www.ippmedia.com/sw/habari/mhitimu-kidato-cha nne-ajitolea-kufundisha-shule-ya-watoto-216
 

Mtu mmoja mmoja kujitolea kwa ajili ya jamii, Tanzania sio habari, tena ni vijana wadogo kabisa mpaka wazee
 

Mngekua mnafanya hivyo kwa kila mmoja, nchi yenu haingejaa matatizo kila kona, Dar haingekua chafu kama ilivyo kwa leo, taarifa kama hizo za mtu kujitolea kuwafundisha watoto 216 waliokosa mwalimu hazingesikika, madudu yote mliyonayo hayangekuwepo.
 
Jirani huyu aliyeweka fence kwenye shamba lake ni settler?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…