Vijana ingieni kwenye ndoa lakini mjue yaliyopo ni kinyume kabisa na matarajio

mapema

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2014
Posts
640
Reaction score
1,881
Nafurahi kufikisha mwaka wa 10 siku ya leo kwenye ndoa. Nilioa kwa vigezo vyote vya dini, yaani ile hakuna ngono kabla ya ndoa.

Ilikuwa ngumu kidogo lakini kwa nguvu ya dini niliweza ingawa mwenzangu sikujua nyendo zake. Na kwa kiasi kikubwa maisha yangu ya ujana sikuruka sana kwa nia njema ya siku nikiwa kwenye ndoa itakua poa.

Baada ya ndoa na uzazi sasa nilichotarajia ni tofauti kabisa na kinachotokea. Imenipelekea kuwa mhuni fulani hivi, mtu wa wanawake sana, malaya kama kawa, safari za mbali kufuata mwanamke, wakati mke yupo karibu yangu kabisa.

Hii ni kwa sababu ya mwanamke kuwa mvivu na mzito kwenye mapenzi, yaani inakuwa rahisi kupata mapenzi nje kuliko ndani. Ndani unaomba mpaka kwa magoti lakini unaambulia patupu.

Nimejuta kutokutumia ujana wangu vyema labda saivi ningekuwa mtulivu. Vijana tumieni ujana wenu vilivyo dini zinazingua muda mwingine.

Hata hivyo bado ndoa ni nzuri.
 
Hiyo ni tabia uliyoamua kuijenga mwenyewe haihusiani na matumizi ya ujana!!!
Kama mke hana tatizo kwanini ukose Unyumba?!! Jitathimin ndg, kabla ya kuleta mawazo hasi hapa jukwaani.
 
Kaka unapiga show kweli.

Au una mwachia shombo shemeji Wetu.
 
Watu wengi baada ya kuoa ,ndio hupata akili za kuoa Sasa[emoji1787],Yaani Kwenye ndoa unaingia mkuku mkuku Zero brain,ukiingia unakuta formation tofauti , kupitia mkeo Ndo unajua kuwa ulitakiwa kutulia kabla ya kuingia humo,

Bahati mbaya Sababu ya kwanza ya kuingia Kwenye ndoa Huwa ni assurance ya UTELEZI,kitu ambacho hakipo ,utelezi ni percent ndogo sana ,the rest ni majukumu mengine ya kujenga familia
 
Nafurahi kufikisha mwaka wa 10 siku ya leo kwenye ndoa.

Nilioa kwa vigezo vyote vya dini , yaani ile no sex before marriage.
Miaka ya zamani, enzi za wazazi wetu, ndoa ilikuwa ni taasisi takatifu (a sacred institution) iliyolenga kujenga msingi muhimu ya jamii imara ambayo ni familia. Ila kwa kizazi hiki chetu cha sasa, sijui ni nini kimeikumba.
 
Sio kila ndoa ina matatizo ya kugongewa kama ya masanja,zingine zipo poa tu
 
Barikiwa
 
Miaka ya zamani, enzi za wazazi wetu, ndoa ilikuwa ni taasisi takatifu (a sacred society) iliyolenga kujenga msingi muhimu ya jamii imara ambayo ni familia. Ila kwa kizazi hiki chetu cha sasa, sijui ni nini kimeikumba.
Zamani ndoa kwa wanawake ilikuwa ni kuzaa na kumfurahisha Mwanaume. Ndoa za sasa kwa mwanamke ni yeye kufurahi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…