LGE2024 Vijana Jitokezeni kwa wingi kupiga kura uchaguzi serikali za mitaa

LGE2024 Vijana Jitokezeni kwa wingi kupiga kura uchaguzi serikali za mitaa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

try me

Member
Joined
Nov 8, 2024
Posts
16
Reaction score
11
Mjumbe wa Baraza Kuu UVCCM TAIFA, Leodger Leonard Kachebonaho alikuwa Mgeni Rasmi Baraza la UVCCM Wilaya ya Karagwe, Baraza lililofanyika tarehe 10/11/2024.

Akizungumza katika Baraza hilo la kikanuni amewataka vijana kujitokeza kwa wingi siku ya tarehe 27 Novemba 2024 kukipigia kura Chama Cha mapinduzi na pia kuendelea kuwa mabalozi wazuri wa wagombea wa CCM katika jamii zetu kwa kuwa ndio Chama Chenye uwezo wa kuwaletea wananchi maendeleo ya kweli.

Katika Hatua nyingine aliwaasa vijana kuanziasha miradi mbalimbali ya kiuchumi itakayoweza kuwakwamua na kujiendesha pasipo kumtegemea mtu mmoja mmoja kuepusha kuwa wafungwa wa kimawazo na kutokuwa na msimamo jambo ambalo halina afya katika siasa za sasa.

Kachebonaho amesema “Kwa kuwaunga mkono hili nitachangia miche ya mazao ya biashara yakiwemo mikahawa, midarasini, mihumla, mifenesi katika shamba lote lakini pia nitawawezesha Ng’ombe wa maziwa (Friesian) watatu (03) ikiwa ni kuhamashisha shughuli za Ufugaji na zaidi kiuchumi kwetu sisi vijana.”

Katika Baraza hilo alipata fursa ya kutembelea eneo ambalo linatarajiwa kujengwa Nyumba ya Katibu wa UVCCM wa Wilaya ya Karagwe ambapo aliahidi kuchangia matofali 500 ya block pamoja na mifuko 50 ya Cement.
 

Attachments

  • IMG_20241114_172026_071.jpg
    IMG_20241114_172026_071.jpg
    289.7 KB · Views: 4
  • IMG_20241114_172026_595.jpg
    IMG_20241114_172026_595.jpg
    349.8 KB · Views: 6
  • IMG_20241114_172026_424.jpg
    IMG_20241114_172026_424.jpg
    416.2 KB · Views: 3
Back
Top Bottom