Vijana kufanya Maandamano kupinga Mkataba wa Bandari kati ya Tanzania na kampuni ya DP World ya Dubai

Vijana kufanya Maandamano kupinga Mkataba wa Bandari kati ya Tanzania na kampuni ya DP World ya Dubai

MzeeKipusa

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2023
Posts
2,705
Reaction score
4,967
Kimeumana!

Nimezipata za chini ya kapeti ya kwamba kuna uwezekano mkubwa wa vijana wa Dsm na wa Dodoma kuingia barabarani weekend hii au Jumatano ijayo kupinga issue ya DP World.

Mambo ni [emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91]

Vijaaanaa vijana vijana tuko tayari kulitumikia, taifa, taifa, taifa kulitumikia Taifa Taifa Tanzania.

Dodoma = Assembling point ni pale Nyerere Squire

Dar = Ni Pale Mnazi mmoja kwenye mnara wa Mashujaa.

=========

UPDATES:

Kijana Deusdedith Soka aitisha Maandamano ya Amani tarehe 19 Juni, 2023 kuanzia Temeke kwenda Ikulu ya Magogoni kupinga mkataba kati ya DP World na TPA pamoja na kupinga Muswada wa TISS kuwekewa kinga ya kutokushtakiwa kwa makosa ya Jinai.

Mkataba wa Bandari.jpg

Deusdedith Soka afanya mkutano na waandishi wa habari kutoa maelezo kuhusiana na route itakayotumika siku ya Jumatatu, Juni 16 kwenye maandamano ya kupinga Mkataba wa Bandari kati ya Tanzaniana Dubai.


Hapa chini ni barua aliyoandika kuhusu maandamano ya Jumatatu 19, Juni 2023

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, aliandika: “@tanpol Msije kujeruhi watu waacheni tudai haki zetu kwa njia ya kistaarabu na kiungwana. Maandamano ya amani, wanasheria kuweni macho kwa askari yeyote atakayevunja Haki za binadamu utashtakiwa mwenyewe.”

Deus 1.jpg

Deus 2.jpg

Hata hivyo, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limetoa tahadahari kwa wananchi kuhusu taarifa za kuwepo na maandamano siku ya Jumatatu Juni 19, 2023 kwenda Ikulu ya Magogoni, Dar es Salaam. Zaidi, soma hapa.
Habari zaidi, soma:
  1. Sakata la DP WORLD: Rais Samia asema Serikali itatafuta mbia wa kuiendesha bandari ya Dar, sasa kuchangia robo tatu ya bajeti ya nchi
 
Nwakumbusha waombe kibali, wakikataliwa iwekwe kwenye records kwamba waliomba wakakataliwa!!!
 
Kama Mtanganyika mzalendo, Mtanzania na raia wa jamhuri ya Tanganyika na ile jumhuri ya Muungano wa Tanzania umejipangaje kushiriki maandamano haya mnamo siku ya Jumatatu?
 
Maandamano wanayaweza wakenya tu sisi kuongea ndio kitu tunaweza
 
Maandamano ya amani ya wana harakati yaliyokuwa yamepangwa kufanyika Dares salaam kupinga mkataba wa bandari kupewa waarabu wa Dubai milele na kudai katiba mpya yamepigwa marufuku kwa kunyimwa kibali na polisi.
Wana harakati hao vijana wamelalama na kulaani kitendo cha kunyimwa kibali cha kufanya maandamano kwani hiyo ni haki yao kikatiba.
 
Demokrasia imekua sana.

Maana hata chawa wakiomba kuandamana kupongeza wanakubaliwa.
 
Kwa Mujibu wa Waratibu wa Maandamano hayo ya Amani , ruti ya Maandamano hayo itaanzia Temeke Mwisho , ambako waandamanaji hao watapita Keko hadi Karume , kabla ya kukunja kona kuingia Mtaa wa Uhuru hadi Mnazi Mmoja , hapo waandamanaji watakunja kushoto kuelekea Kisutu ambapo msafara huo utakunja kulia hadi Posta na kukata kona ya Mwisho kuelekea Kivukoni .

Ikumbukwe kwamba Katiba ya Tanzania inatoa ruhusa kwa wananchi wake kufanya Maandamano ya Amani .

Angalizo : Waandamanaji hawatatakiwa kubeba silaha yoyote ile na Watakaguliwa kabla ya kujiunga kwenye maandamano , kinachoruhusiwa ni Majani na Mabango tu .

FB_IMG_1686827371834.jpg
 
Back
Top Bottom