Vijana kufanya Maandamano kupinga Mkataba wa Bandari kati ya Tanzania na kampuni ya DP World ya Dubai

I had to do a double take on this one!

Keshokutwa, Jumatatu, kuna watu wamepanga kuandamana jijini Dar kupinga mkataba wa bandarini na kupinga muswada/ sheria mpya ya TISS.

Ngoja nicheke kwanza….bwahahahaaaa.

Kwa niwajuavyo Watanzania, hapo ni kujisumbua na kupoteza muda tu.

Watanzania sisi ni waoga sana. Hatuna mwamko wowote ule ulio wa maana kwenye kupigania maslahi yetu.

Sisi ni watu wa kuburuzwa buruzwa tu kama kondoo.

Tunatoa heshima ya ki Mungu kwa viongozi wetu. Hata wakikosea hatuwatupii lawama zinazostahili.

Viongozi wakikosea, lawama hupewa washauri wa hao viongozi.

Kiujumla sisi ni waoga, ni makondoo, ni mafisi, wasahaulifu, na vivumishi vingine vinavyoelezea tulivyo.

Ukweli ni kwamba hili suala la bandari upepo wake ushaanza kupita. Kufikia mwisho mwa wiki ijayo, tayari litakuwa lishakua historia.

Sidhani kama hiyo Jumatatu kutakuwepo na mwitikio wowote ule wa maana kwenye hayo maandamano.

Sana sana wataojitokeza ni baadhi tu ya wanaharakati wa mitandaoni na vibango vyao viwili vitatu.

Kiufupi itakuwa ni kupoteza muda tu.

Ila, ikitokea kinyume na ninavyodhani, basi sitokuwa na hiana kukubali kuwa nilikosea.

Tusubiri tuone kitachojiri hiyo Jumatatu.

 
Kwani waliokamatwa kwa kuandamana wamehamasishwa na nani? Naona jamaa aliomba ulinzi wake peke yake!
 
Haya maandamano yameishia wapi MzeeKipusa ?😂
 
Haya maandamano yameishia wapi MzeeKipusa ?[emoji23]
Mimi huwa naona mambo kabla hayajatokea. Kiufupi mambo sio shwari kabisa!.

Vyombo vya ULINZI , USALAMA na POLISI , vijipange sana.


Note: Polisi sio chombo cha Ulinzi na Usalama. Vyombo vya Ulinzi na Usalama ni USALAMA WA TAIFA pamoja na JWT


POLISI ni Raia tu kama sisi, ni Sawa na JKT tu ( Raia wanaolipwa mishahara na Serikali kwà ajili ya kutulinda sisi na mali zetu )

POLISI ni Sawa na wale walinzi wa nzego...ambao huchangiwa af5 5 KILA mwezi.
 
Je ulitokea?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…