Vijana kufatilia zaidi mpira kuliko mambo muhimu yanayoathiri nchi tatizo ni nini?

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Hapa chini nimeweka video ya wana Dar es Salaam wakisherehekea ushindi (kombe), ambapo wengi wao ni vijana.

Jana taifa lilikuwa na jambo muhimu sana kwa mustakabali wa vizazi na vizazi, jambo lililogusa Bandari ambazo ndizo kiini cha uchumi na heshima ya nchi.

Mpira na furaha ni muhimu sana kwa maendeleo ya nchi, ila most of these young men they don't care about their future. Wanajua ukienda kazini na kurudi basi umemaliza.

Cha ajabu tukio la kupokea kombe limeteka nyoyo na macho ya vijana kuliko suala la Bandari. Je, tutafika?

Ni ujinga wa kurogwa au kurithi?

Kuna mdau aliwahi kuniambia hizi klabu za Simba na Yanga zipo kwa ajili ya manufaa ya viongozi uchwara hapo kwenye siasa. Yaani iko hivi inaweza kutokea jambo muhimu la kitaifa wananchi wakalipigia kelele sana sasa hao viongozi uchwara wakiona hivyo wataingiza agenda yoyote ile ya usimba na uyanga ili kuwapunguza makali.

Refer jambo la jana kulikuwa na haja gani kwa Yanga kufanya hiyo parade wakati ata fainali ya FA hawacheza!? Yaani fainali iko baada ya siku moja kutoka jana kisha ichezwe alafu unawapigisha parade wachezaji hivi inaingia akilini kweli, bila shaka tunarudi kule kule hilo jambo ilikuwa ni kuwapumbaza watanzania wasifuatilie masuala muhimu kule bungeni.

Inshu ni nyingi sana zinatokea na zinazimwa na usimba na uyanga. Kama we ni mfuatiliaji wa mambo nadhani unatambua hilo. Ila muhimu zaidi sisi watanzania tumekalia ma mipira na ngono muda wote tu.
 
Kwahiyo ulitaka watu wote wafuatilie Bunge kwenye tv kwa kujifungia ndani? mwisho utaleta na picha ya kuwaonyesha watu wakiwa kwenye harakati zao za utafutaji kua nao hawakua wakifuatilia bunge, wewe uliyefuatilia na wao ambao hawakufuatilia,sasa hivi wote mnazo information sawa kwa kilichojadiliwa,kumbuka teknolojia ya kupashana habari ipo active na rahisi kumfikia mtu popote alipo.
 
Huo umati ndio mtaji wa CCM kuendelea kuwa madarakani!
 
Mimi ni mwanaSimba.

Sioni tatizo. Maana hata wangeacha kwenda kushangilia timu yao na wote mkabaki kukodolea macho azimio la Bunge, bado msingebadili chochote.

Mara nyinggine shadadia kinachokupa furaha. Hao wamefurahi sana jana. Sisi tuliobaki kuwasikiliza Mabwenyenye huko bungeni tumeambulia sonona.
 
Vijana wengi hawafatilii siasa, huo mjadala wa bandari upo humu jf na huko twitani.

Huenda huo umati wote hapo ni wachache wanajua kua bandari iko rehani achilia mbali hata wanaojua nini kinaendelea
 
Hapa chini nimeweka video ya Wana Dar es salaam wakisherehekea ushindi (kombe ).
Wengi wao ni vijana.
Jana taifa lilikuwa na jambo muhimu sana kwa mustakabali wa vizazi na vizazi, jambo lililogusa Bandari ambazo ndizo kiini cha uchumi na heshima ya nchi.
Mpira na furaha ni muhimu sana kwa maendeleo ya nchi, ila most of these young men they don't care about their future. Wanajua ukienda kazini na kurudi basi umemaliza.
Cha ajabu tukio la kupokea kombe limeteka nyoyo na macho ya vijana kuliko suala la BANDARI.
Je, tutafika?
Ni ujinga wa kurogwa au kurithi?
View attachment 2653730
Acha ujinga.. Swala la bandari linapingwa zaidi na mafisadi pamoja na wezi waliokuwa wananufaika na mfumo mbovu wa bandari uliopo sasa.

Wanapitisha mizigo yao bila kulipa ushuru au kodi wakishirikiana na baadhi ya viongozi waliopo hapo bandarini.

Hii vita ya bandari naifananisha na ile vita ya watu wa vyeti feki serikalini, ambapo waliokuwa wananufaika na mfumo ule wa vyeti feki ndio waliokuwa wanaongoza kwa kupiga kelele mitandaoni, na magazetini kuhusu hatua ile ya kuwaondoa wenye vyeti feki makazini.

Lakini pia hili swala linafanana pia na ile vita ya wauza madawa ya kulevya, ambapo wauzaji madawa waliunda mtandao wao wenye nguvu mitandaoni, na magazetini ili viwasaidia kupiga vita kile kilichokuwa kinafanywa na serikali dhidi yao (wauza madawa)

Hii ni sawa na watu wanaoiba dukani miaka na miaka, afu mwenye duka anapoamua kufunga kamera katika duka lake wale waliokuwa wananufaika na wizi waanze kulalamika kwamba mwenye duka ameshindwa kuwaamini na kuwavunjia heshima ndo maana amefunga kamera, na longo longo zingine.

Binafsi nashauri raisi asisitishe swala hili maana lina faida kubwa kwa miaka ijayo, hawa waliozoea kuitumia bandari yetu kama shamba la bibi kwa kupitisha vitu vyao (bila kulipa kodi) watafute kazi zingine za kufanya, maana ile janja janja yao itakuwa imefika mwisho.

Hatuwezi kuruhusu huu ujinga uendelee miaka na miaka au maraisi kuwa na kazi ya kubadilisha wakurugenzi wa bandari kila siku.

Inawezekana lile kundi linalonufaika na mifumo ya sasa likalipa baadhi ya wanasiasa uchwara pesa, ili kuwapigania na kuwatetea lkn katika hili naamini watashindwa tu.
 
Shida nyie maafande mnaowataka vijana wapaze sauti na wapiganie haki zao ndio nyie nyie mnapewa Silaha na Oda za kuwala vichwa.
 
Kuna mdau aliwahi kuniambia hizi klabu za Simba na Yanga zipo kwa ajili ya manufaa ya viongozi uchwara hapo kwenye siasa. Yaani iko hivi inaweza kutokea jambo muhimu la kitaifa wananchi wakalipigia kelele sana sasa hao viongozi uchwara wakiona hivyo wataingiza agenda yoyote ile ya usimba na uyanga ili kuwapunguza makali.

Refer jambo la jana kulikuwa na haja gani kwa Yanga kufanya hiyo parade wakati ata fainali ya FA hawacheza!? Yaani fainali iko baada ya siku moja kutoka jana kisha ichezwe alafu unawapigisha parade wachezaji hivi inaingia akilini kweli, bila shaka tunarudi kule kule hilo jambo ilikuwa ni kuwapumbaza watanzania wasifuatilie masuala muhimu kule bungeni.

Inshu ni nyingi sana zinatokea na zinazimwa na usimba na uyanga. Kama we ni mfuatiliaji wa mambo nadhani unatambua hilo. Ila muhimu zaidi sisi watanzania tumekalia ma mipira na ngono muda wote tu.
Wananchi wana ratiba zao, Wadau wa bandari na wanabandari pia wana ratiba zao, sasa hapo shida ipo wapi?
Yaani ulitaka wananchi waahirishe shughuli zao kama wananchi wakafuatilie mambo ya bandarini?
 
Hapana mkuu sijamanisha hivyo, samahani kwa kutonielewa.

Upo sahihi mkuu
 
Ila watanzania wengi mambo ya mpira yamewakaa vichwani Sana.
 
Back
Top Bottom